Wadau wa afya wakabidhi Klinik waliojenga kwa jitihada zao na wananchi. Hafla hiyo fupi ya kukabidhi jengo la zahanati imefanyika kijiji cha Mahhahha kata ya Endamariek. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Godfrey Luguma pamoja na ndugu Erik Haes walikata utepe kwenye klinik na baadae mdau huyo kukabidhi jengo hilo kwa Halmashauri.
Ndugu Erick Haes amesema amejenga jengo hilo la klinik kwa ushawishi wa Mhe. John Lucian ambaye ni diwani wa kata ya Endamariek. Amesema wao wamejikita katika kusaidia jamii na shughuli zao wameanza kufanya nhini Angola. Mdau huyo ndugu Erik amewapongeza wananchi wa Mahhahha kwa ushirikiano mkubwa walitoa wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa kliniki hiyo. Ndugu Erik amesema wingi wa watu kijiji wanachotoka huko kwako ni watu 3000 kama kijiji cha Mahhahha.
Wamefanikiwa kuchangangisha fedha huko kwao kwa kuanda michezo ya mbio za kukimbia msituni, fedha ambazo zimetumika kwa ujenzi wa klinik hiyo katika kijiji cha Mahhahha. Ndugu Erik amefurahi kuona kwamba kituo hicho kimepewa jina la aliyekuwa mke wake GERT MAES MEMORIAL CLINIK-MAHHAHHA. Ambaye alifariki mwaka 2014 na alikuwa anajihusisha katika shughuli za kusaidia jamii. Amesema malengo yao ni kuona kliniki hiyo inaendelea kukua na baadae kupata hadhi ya kuwa kituo cha afya. Ndugu Erik Haes na mke wake wa sasa bi, Els Hennebel wamesema wataendelea kushirikiana na watu wa kijiji cha Mahhahha.
Mhe. John Lucian amewapongeza wananchi wa Mahhahha kwa kujitokeza kujenga klinik hiyo. Amesema wanakijiji wamejitolea kununua eneo ambalo jengo hilo la klinik limejengwa. Mhe. Lucian amesema jengo hilo lina sehemu ya wagonjwa ya nje, kuna sehemu ya kujifungua kwa wakinamama. Amesema katika ujenzi huo amesimamia fedha zilizotolewa kwa mradi huo pamoja na kujitolea magari yake bure kwa ajili ya mradi huo. Mhe. Lucian amesema jengo limetengenezewa miundo mbinu ya maji na umeme ambayo imebaki kuunganishwa, na lina thamani ya zaidi ya million tisini. Mhe. Lucian amesema wameshaanza kujenga msingi wa jengo la nyumba ya daktari na nesi jengo ambalo litakuwa two in one. Ameomba wanakijiji kufanya utaratibu wa kutafuta matofali kwa ajili ya jengo hilo na wao watatafuta namna ya kumalizia. Mhe Lucian ameomba kutunza klinik hiyo ili miundo mbinu ya majengo hayo isije kuharibika.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji Ndugu Godfrey Luguma amewashukuru wafadhili kwa kujitolea kujenga jengo la afya ili kusogeza huduma za afya karibu. Amewapongeza wananchi na Mhe. Lucian kwa kutafuta eneo la mradi na kwa jitihada mbalimbali walizofanya kukamilisha ujenzi huo.
Awali katika risala ya wananchi wa kijiji cha Mahhahha iliyosomwa na Mtendaji wa kijiji ndugu Emmanuel Izrael wamesema kukamilika kwa kliniki itakuwa msaada mkubwa kwao. Kliniki hiyo itasaidia wakazi zaidi 1900 wa kijiji cha Mahhahha na wananchi wa vijiji vingine vya karibu. Wameomba wadau hao marafiki wa Mhe Lucian kuendelea kusaidia miundo mbinu mingine ya kijamii katika kijiji chao kama ujenzi wa nyumba za madaktari na wauguzi lakini pia vifaa tiba.
Jengo la Klinik liliokabidhiwa kwa Halmashauri.
Picha ya pamoja ya marafiki wa Mhe. Lucian; Kaimu mkurugenzi, Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya, Mhe. Lucian na uongozi wa kijiji cha Mahhahha.
Kiongozi wa kijiji akitoa shukrani kwa wadau waliojitolea kujenga jengo la klinik.
Wananchi wakisikiliza mkutano uliofanyika mbele ya klinik ya kijiji cha Mahhahha.
Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya kukabidhi jengo la klinik kwa Halmashauri.
Wananchi wakicheza ngoma katika hafla ya kukabidhi jengo la Kliniki kwa Halmashauri.
Mhe. Lucian akionesha wataalam miundo mbinu ya jengo la klinik.
Mhe. Lucian akionesha vyumba vya jengo kwa Kaimu Mkurugenzi Ndugu Luguma.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa