Mashabiki wa timu ya simba wilaya ya Karatu wamejitokeza kuchangia damu salama na kufanya usafi katika kituo cha afya cha Karatu (Double d). washabiki hao kindaki ndaki wamefanya shughuli hizo za kijamii kama sehemu ya kuadhimisha siku ya simba, ambayo hutumika kutambulisha wachezaji wapya, pamoja na jezi mpya watakazotumia msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara.
Afisa mipango miji ndugu Pastory Rwebangira amepongeza washabiki hao wazalendo wa timu ya simba kwa moyo wao walioonesha kufanya usafi na kuchangia damu kituo cha afya Karatu. Amesema eneo hilo la nyuma ya hospitali lilikuwa limeshakuwa kichaka na tishio lakini kwa usafi uliofanywa na mashabiki wa simba eneo linapendeza na linavutia. Juhudi zilizofanywa na washabiki wa timu ya simba ni jitihada za kuimarisha na kuifanya wilaya yetu kuwa safi, ameomba mashabiki hao kuendelea kujitokeza kwenye usafi, pindi watakapoalikwa hasa siku jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya usafi wa mazingira.
Mashabiki wa simba wakifanya usafi kituo cha afya Karatu
Naye mganga mkuu wa kituo cha karatu (Double d) Dkt. Vicent Gyunda ameshukuru mashabiki wa simba Karatu kwa moyo wao. Amesema michezo ni afya na kitendo walichofanya ni chakuingwa na kinapaswa kuigwa na watu wengine. Dkt. Vicent amesema kinga ni bora kuliko tiba hivyo kitendo cha kufanya usafi ni kinga dhidi ya maradhi mbalimbali yanayosababishwa na uchafu, amesema anaamini hata watani wao wa jadi wataiga kitendo waliochofanya. Ameshukuru mashabiki hao wa simba kwa uchangiaji wa damu amesema kituo cha afya Karatu ni kituo kimbilio kwa wakinamama wajawazito. Amesema kituo kinafanya upasuaji kwa wakinamama wajawazito wanaoshindwa kujifungua kwa njia za kawaida takribani 40 kwa mwezi. Hivyo kuna uhitaji wa akiba ya damu salama, ili kuendelea kuhudumia wagonjwa katika kituo hicho.
Mashabiki wa simba wakifyeka majani kituo cha afya Karatu.
Naye shabiki wa simba Ndugu Eligard Chilonga amesema maaumuzi waliochukua ya kufanya usafi na kuchangia damu ni kielelezo kwa kila mtu kwamba wameamua kuonesha namna mpya ya usherehekeaji wa siku ya timu ya simba ( wekundu wa msimbazi). Tukio hilo litakuwa endelevu na huo ndio mwanzo tumeanza kuandikisha majina ya wanachama mashabiki wa simba wilayani Karatu ili wakati ujao tufanye kitu kikubwa zaidi. Amesema kwa majina waliyoandikisha ya wanachama ni 80 wanataka wafikishe idadi ya wanachamaa 200 ili watimize adhima yao ya kufungua tawi la simba Karatu.
Naye Ndugu salumu Sevingi mshabiki wa simba amewataka washabiki wa simba kujitokeza kushangilia timu yao kwa nguvu msimu huu wa ligi kuu. Amesema juzi ilikuwa send off ya watani wao lakini leo ndio sherehe yenyewe ya harusi. Kila kitu wanachokifanya simba ni darasa kwa watani wao wa jadi, hivyo amewaomba kuonesha utofauti katika kusherekea siku yao ya kutambulisha kikosi kipya cha timu ya simba, kitakachocheza na timu ya Power Dynamo majira ya saa kumi na moja na nusu alasiri. Sherehe hizo za utambulisho wa kikosi cha timu ya simba zitafanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salam.
Mashabiki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kazi, simba nguvu moja
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa