Watalii kutoka chuo cha Calfonia cha chini marekani wametembelea kituo cha utalii cha kitamaduni wa ki iraq cha Moya kilichopo Karatu. Wamepata nafasi pia ya kuongea na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu, na kujadili mambo ya kijamii pamoja na kiuchumi. Karatu ni lango la utalii kwa hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro, hifadhi ya ziwa Manyara na hifadhi ya Serenegeti.
Moya ni kituo cha utalii wa kitamaduni wa kabila la wairaq wanaopatikana Karatu. Kituo hicho cha utalii kinazungumzia kuhusu asili ya wairaq, ngoma za asili ya Iraq lakini pia kupata nafasi ya kula vyakula vya asili vinavyopikwa na wairaq. Kituo hicho kinajihusisha na kuuza bidhaa za kitamaduni kama heleni na bangili na mashuka ya kimasai yanayopatikana katika kituo hicho cha utalii. Watalii hao walipata wasaha wa kutoa shuka za kimasai kumi kwa wajane katika eneo hilo pamoja na kutembea eneo la shule ya watoto wadogo lilopo Fao. Eneo hilo la shule lipo kitongoji cha Fao katika mji wa Karatu. Katika kituo hicho watalii walitoa vifaa mbalimbali kwa watoto wa shule ya Kifaru Healthy children centre.
Mwenyekiti wa halamashauri Mhe. Jublate Mnyenye amewashukuru watalii hao kwa kuja kutembelea karatu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Mhe. Jublate Mnyenye amesema mazungumzo waliyofanya katika ukumbi wa halmashauri yatawasaidia kuwapatia ufumbuzi kwa changamoto zinazowakabili kama Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Mhe. Mnyenye amewaomba watalii hao kuwa mabalozi wazuri kwa yale waliyojifunza kutoka karatu. Wageni hao walipata taarifa namna serikali ilivyowekeza katika sekata ya elimu sekta ya afya sekta utalii na sekta ya maendeleo ya jamii.
Afisa utalii wa wilaya ya Karatu bi, Salome Kivuyo amesema katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo wamejenga uelewa wa kufahamu fursa mabalimbali zinazowazunguka wajasiriamali hao katika eneo la Karatu.Bi,salome amesema serikali imejikita katika kuwapa elimu ya uelewa namna ya kufanya kilimo cha mbogamboga na kuweka bidha katika vifungashio vilivyowekwa alama. Serikali inawapa elimu wananchi njia bora za ufugaji a kuku na mifugo inayoendana namahitaji ya soko. Amesema serikali imejikita katika kutoa elimu kwa wajasiriamali ili waweze kutumia elimu hiyo kujielimsha na kufanya shughuli zao za ujasiriamali.
Mganga kiongozi wa kituo cha afya Karatu Dkt. Vicent Gygunda amesema kituo hicho cha afya kinahudumia kinamama wajawazito wanaojifungua kawa njia ya operesheni thelathini mpaka ishirini kwa mwezi. Lakini kinapokea wakinamama wajawazito kati ya miambili mpaka mia tatu wanaojifungua kwa njia ya kawaida. Dkt vicent amesema kituo kina vitanda athelathini na mbili tuu, na bado kituo kinatoa huduma ya kiuangalizi kwa wakinamama wajawazito mia nne na thelathini na nne. Changamoto ya kituo hicho cha afya ni kwamba miundo mbinu ya sekta ya afya haiendani na mahitaji ya wagonjwa wanaohudumiwa katika kituo hicho cha afya.
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Calfonia parofessor Frank Lin amesema matatizo ya ndani ya jamii yanahitaji ufumbuzi kutoka katika jamii yenyewe husika. Amesema ni vyema serikali ikahusisha wanafunzi na wadau wengine katika tafiti za matatizo yanayowakabili ili yaweze kupatiwa ufumbuzi wa kitaalamu. Amesema amefurahi kuona vivutio vinavyopatikana katka wilaya ya Karatu na amejisikia kama yupo nyumbani. Amesema ni vyema kuwahusisha wadau wote wa utalli ili kupata ufumbuzi wa changamoto zianazokabili sekta ya utalii Karatu. Majadala huo umewapa ufahamu ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizotajwa ili kujenga uchumi imara.
Watalii wakipata maelezo ya alama mbalimbali katika Nyumba ya Utalii wa ki iraq Moya Karatu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa