Afisa elimu sekondari ameendelea na ukaguzi wa shule za sekondari upande wa tarafa ya Endabash. Katika ziara hiyo amezungumza na kuwaasa walimu juu ya mbinu za ufundishaji, na ufuatiliaji wa wanafunzi ili kupata matokeo chanya. Shule tatu zilizotembelewa ni Marang, Orboshan na Kansay.
Bi,Kalista Maina amesema kuwa na andalio la kazi ni muhimu kwa sababu ndio dira inayokuongoza katika ufundishaji. Amesema ni rahisi sana kutoka nje ya malengo uliojiwekea kufundisha somo kama huna andalio la somo. Bi Maina amesema hayo baada ya kukuta walimu hawana maandalio ya masomo na wengine kuandika maandalio hayo kwa kuruka ruka bila kufuata utaratibu. Amesema hapo ndipo makosa ya ufundishaji yanapoanza na matokeo yake wanafunzi wanafeli katika mitihani.
Ameipongeza shule ya Marang kwa kushika nafasi ya 12 kati ya shule 32 za Wilaya na kwa ngazi ya mkoa imekuwa shule ya 204 kati ya 226. Shule ya Orboshani imekuwa shule ya 8 kati ya 32 ngazi ya za wilaya na ngazi ya mkoa imekuwa shule 84 kati ya shule 226. Shule ya kansay imekuwa ya 22 kwa ngazi ya wilaya kati ya shule 32 na kwa ngazi ya mkoa imekuwa 187 kati ya shule 226. Lakini pia amemuelekeza Mkuu wa shule Marang kwenda na mwalimu wa baiolojia kwenda kutoa maelezo kwa mwajiri baada ya kupata âFâ masomo yote kwenye mtihani wa Moko. Amesema walimu wa Historia na Geografia wataandika maelekezo kujieleza sababu ya watoto kufanya vibaya masomo yao katika mtihani wa Moko kidato cha nne.
Bi, Maina amebaini walimu wanaofanya kazi kwa muda mrefu bila kupata nafasi ya kuchaguliwa kusimamia mitihani. Amesema lazima kuwe na uwiano sawa wa kuchagua walimu wa kwenda kusimamia mitihani ya taifa. Bi. Maina amekutana na walimu ambao wamekaa miaka zaidi ya saba bila kusimamia mwaka hata mmoja mitihani ya taifa.
Afisa elimu sekondari akiwa anafanya ukaguzi wa vifaa vya kiutendaji vya mwalimu.
Afisa elimu taaluma ndugu Robert Sijaona amesema ualimu ni dhamana ni vyema walimu wakaitambua dhamana waliopewa. Mada za masomo zipo kwa mpangilio maalumu ni lazima mwalimu afuate utaratibu wa kufundisha. Walimu tuwaelekeze wanafunzi utaratibu mzuri wa kuhifadhi notsi za masomo kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne. Hiyo itamsaidia na kumrahisishia mwanafunzi wakati wa kusoma na kujikumbusha. Amesema ni vyema walimu wakakaa vikao siku ya ijumaa ili kujitathimini shughuli za kitaaluma. Hiyo itasaidia katika uwajibikaji ili kupunguza dosari za ufundishaji.
Naye afisa takwimu Sekondari Bi, Brenda Mlay amesema ni vyema walimu tukubali kuwajibika, kumekuwa na tabia ya walimu kujitokea tu kwenye vituo vya kazi. Ametoa maelekezo kila shule kuwa na daftari linaonesha taarifa za kutoka kwa mwalimu. Agizo hilo ni kwa walimu wote ili kuzuia ruhusa na kujiondokea kiholela kwa walimu katika vituo vya kazi. Ziara hiyo imebaini baadhi ya walimu kutokuwepo kwenye vituo vya kazi na hakuna fomu walizojaza kuomba ruhusa shuleni na wilayani.
Afisa akiwa na mwalimu akiangalia na kukagua mafaili mbalimbali
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa