Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amefanya ziara katika kituo cha afya kambi ya simba. Mhe Gambo amekagua miundo mbinu ya kituo hicho cha afya pamoja na kuzungumza na wafanyakazi na wananchi walijitokeza kumlaki.
Mhe. Gambo amesema kazi ya serikali imeonekana kulikuwa na zahanati kambi ya Simba na baadae zahanati imepanda hadhi kuwa kituo cha afya. Taasisi ya hifadhi ya Ngorongoro imekuwa taasisi ya mfano kwa kusaidia huduma za afya wilayani Karatu. Amesema kutoka kituo cha afya cha Kambi ya simba mpaka kufika kwenye hospitali ya wilaya ni umbali wa km 35 ni umbali mrefu sana kwenda kupata huduma za afya. Mhe, Gambo amesema tunapokuwa na huduma nzuri za afya katika kata zetu zinaondoa kero ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya. Amesema hayo ni maelekezo ya serikali na ndio ilani ya chama cha mapinduzi.
Mhe. Gambo amewapongeza wananchi wa kata ya mbulumbulu kwa juhudi zao za kujiletea maendeleo. Amewapongeza Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutoa kiasi cha shilingi million 40 kujenga jengo la wodi ya wazazi kipindi cha nyuma na mamlaka hiyo pia imetoa kiasi cha shilingi million 20 kukamilisha ujenzi wa jengo la Exray. Amesema Exray ni mhimili wa kituo cha afya. Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuchangia Million 5 kukamilisha ujenzi wa wa jengo la Exray na wananchi kutoa kiasi cha million mbili kwenye account yao ili kukamilisha ujenzi wa jengo hilo katika kituo cha afya Kambi ya simba.
Muonekano wa kituo cha afya Kambi ya Simba kwa upande wa mbele
Mhe. Mrisho Gambo amesema tuna rais wa pekee sana Tanzania, amesema awali wilaya ya Karatu ilikuwa inapata kiasi cha million 135 za dawa lakini sasa wilaya inapata kiasi cha million 480 kwa ajili ya dawa tuu. Amesema kwa ngazi ya mkoa Arusha ilikuwa inapata kiasi cha shilingi billion 1.2 kwa mwaka lakini sasa kiasi cha fedha kinachotolewa ni billion 6 kwa mwaka mkoa wa Arusha. Mhe. Mrisho Gambo ametoa rai kwa MSD kumalizia kufanya ukarabati vifaa vinavyohitajika katika majengo ya kituo cha afya Kambi ya Simba ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi mzuri.
Awali katika taarifa ya Daktari kiongozi Deodatus John wa kituo cha afya Kambi ya Simba amesema ujenzi wa kituo cha Afya Kambi ya Simba umetumia force account na ujenzi ulikamilika rasmi april 2018. Dkt John amesema kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya, wagonjwa walikuwa wanapokea wagonjwa kati ya 800 mpaka 1400 kwa mwezi. Idadi imeongezeka baaada ya kukamilika kwa kwa mradi na kufikia idadi ya wagonjwa kati ya 1500 mpaka 1800 kwa mwezi. Kituo cha afya kambi ya simba kimegharimu kiasi cha million 600. Kijiji cha kambi ya simba kimechangia kuchimba misingi ya ujenzi; kusawazisha eneo, kununua matanki ya maji, kununua mabomba ya maji, kugonga na kupakia mawe, kupasua kokoto, na kusawazisha maeneo ya ujenzi.
Mkuu wa mkoa Mhe. Mrisho Gambo mwenye kofia, akikagua vifaa na kupewa maelezo na watendaji wa wilaya katika kituo cha afya Kambi ya Simba
Dkt John amesema Halmashauri ilichangia lori la mafuta kwa ajili ya kuchukua mchanga, kutoa gari kwa ajili ya usimamizi wa mradi. Amesema ujenzi wa mradi wa afya kituo cha kambi ya simba; TAMISEMI walitoa million 500, wananchi million 64 laki tano na elfu ishirini na nne. Halmashauri ilichangia million 86 laki sita na elfu tisini na tano. Dkt john amesema miradi mipya ni jengo la upasuaji, jengo la maabara jengo la wodi ya watoto, nyumba ya mtumishi, jengo la kufulia, jengo la kuhifadhi maiti, tanki la kuhifadhi maji, tanuru la kuchomea taka na njia za kuunganisha majengo. Majengo yaliyofanyiwa ukarabati ni jengo la wgonjwa wa nje, wodi ya wazazi, wodi ya wanaume na wanawake, jengo la klinik. Dkt John amesema vifaa tiba vilivyopokelewa ni 33 kati ya 46. Vifaa hivyo vinathamani ya million 331 laki tano na elfu arobaini na mianne sabini. Dkt John amesema ufuatiliaji wa vifaa kwa meneja wa MSD-Moshi unaendelea ili kuhakikisha vifaa ambavyo havijafika vinafika,
Dkt john amesema kuanzia mwezi wa tano mwaka huu huduma ya upasuaji mkubwa imeanza kutolewa. Hadi sasa upasuaji kwa wakinamama wajawazito wanne umefanyika. Dkt john amesema pamoja na mafanikio hayo bado wanaupungufu wa wataalamu kama mtaalamu wa mionzi, uhaba wa nyumba za watumishi na kituo hicho cha afya hakina uzio
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa