Na Tegemeo Kastus
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI amefanya ziara ya siku moja katika wilaya ya karatu. Katika ziara hiyo ameambatana na mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karatu na ametembelea na kukagua miradi mitatu ya maendeleo.
Mhe. Jafo ameambatana na mbunge wa jimbo la Karatu Mhe. William Qambaru pamoja na mbunge wa viti maalum wilaya ya Karatu Mhe. Cecilia Pareso. Katika mradi wa hospitali ya wilaya ya Karatu alioenda kujionea hatua za ujenzi wake Mhe. Sulemani Jafo amesema ni lazima watendaji kujenga majengo kwa ukamilifu na kuhakikisha wanunua vifaa kulingana na mahitaji ya ujenzi. Amesema miradi mingi inashindwa kwa sababu watu wananunua vifaa vingi ambavyo baadae vinakosa uhitaji. Amesema million 100 iliyotolewa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro itumike vizuri na iendane na mahitaji ya ujenzi wa majengo.
Mhe. Jafo amesema serikali imetenga million 500 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya. Ametoa maelekezo kwa watendaji kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa vizuri, amesema ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Karatu ni kipaombele kikubwa kwa serikali. Amesema ujenzi wa hospitali ya wilaya utakapokamilika, itawekwa vifaa vingi vya kitabibu ili watu waweze kupata matibabu ya uhakika.
Mhe. Jafo amepongeza Halmashauri ya Karatu kwa ukusanyaji wa mapato pamoja. Lakini pia kwa kuhakikisha fedha zinazokusanywa zinapelekwa kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo ya wananchi badala ya fedha hizo kutumiwa na madiwani kufanyia posho za safari.
Mhe. Selemani Jafo amepongeza Halmashauri ya Karatu kwa uthubutu wa kutumia fedha za ndani kiasi cha million 300 kujenga soko la mji wa Karatu. Mhe Jafo ametoa maelekezo mpaka mwezi tatu tarehe 30 ujenzi wa vizimba ukamilike ili wafanyabishara warudi kufanya biashara ndani ya eneo la soko. Amemulekeza Mkurugenzi Mtendaji wale wafanyabishara waliokuwa wanafanya biashara awali ndio warudishwe kwenye soko. Amesema ujenzi wa soko la Karatu mjini ameuchukua kama ajenda maalumu. Amesema ataangalia namna gani soko hilo linaweza kuwa zuri.
Mhe. Jafo amemuelekeza mkuu wa Mkoa wa arusha Mhe.Mrisho Gambo kuunda tume kufuatilia madai moja ya msambazaji wa vifaa Mushi brothers anayeidai Halmashauri million 81 wakati wa ujenzi. Lengo la tume hiyo ni kujiridhisha uhalali wa deni hilo na kisha kumpa taarifa Mhe. Jafo kwa hatua zaidi.
Mhe Jafo amesema amefarijika sana kwenye miradi aliyotembelea Karatu, ameona namna ya viongozi wa Arusha walivyojizatiti katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Ameusifia uongozi wa mkoa wa Arusha, Mhe. amesema mkuu wa Mkoa wa Arusha anatendea haki nafasi yake, Mhe. Jafo amempongeza pia mkuu wa wilaya ya Karatu kwa utendaji wa kazi nzuri amesema ni moja ya wakuu wa wilaya wenye umri mkubwa lakini anajituma sanaa
Amesema kituo cha Afya Kambi ya simba ni moja ya kituo cha mfano Tanzania. Ameongeza kusema ametembelea kituo cha Afya kambi ya simba ili kutoa pongezi. ubora wa majengo ya kituo cha afya kambi ya simba ni sawa na hospitali ya wilaya kwa baadhi ya wilaya nyingine. Ametaka hospitali ya wilaya ujenzi wake uwe mzuri kama ulivyo wa kituo cha kambi ya simba. Amesema Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya kazi nzuri sana katika kipindi cha uongozi wake ameomba wananchi kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mhe. Selemani Jafo katikati akiwa katika eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Karatu kijiji cha changarawe
Mhe, Jafo mesema katika nchi hii kulikuwa na vituo 118 vinavyoweza kutoa huduma ya upasuaji. Awamu ya tano kuna vituo takirbani 400 ambavyo vinaweza kutoa huduma ya upasuaji nchi nzima. Amesema hata maamuzi ya kuanza kujenga majengo ya hospitali za wilaya 70 nchi nzima kwa awamu ya kwanza si jambo rahisi, kiasi cha fedha billion 100.5 zimetolewa kwa ujenzi wa hospitali hizo za wilaya. Mambo haya yanatekelezeka kwa sababu ya uongozi mzuri, miradi hii inahitaji fedha nyingi na inahitaji uthubutu. Mhe Jafo ametoa wito kwa watendaji kuacha masihara katika kuhudumia wananchi amewataka kufanya kazi kama ibada.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa