Na Tegemeo Kastus
Waziri wa Nchi Ofis ya Rais tawala za mikoa serikali za mitaa TAMISEMI ametembelea na kukagua miundo mbinu ya shule ya Sekondari Karatu. Mhe. Selemani Jafo ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karatu.
Mhe. Jafo ameambatana na mbunge wa jimbo la Karatu Mhe. William Qambaru pamoja na mbunge wa viti maalum wa wilaya ya karatu Mhe. Cecilia Pareso. Mhe. Jafo amesema zaidi ya shilingi trillion 1.31 toka mwaka 2016 mpaka January 2020 zimetolewa kwa ajili ya mpango wa elimu bila malipo. Amesema uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu umefanyika kwa shule za msingi shule za sekondari za kawaida, Mhe. Jafo amesema katika kuainisha shule kongwe zinazohitaji ukarabati walipata shule 89. Mpaka sasa shule 64 zimeshafanyiwa ukarabati nchi nzima, amesema namna shule hizo zilivyokuwa na sasa hivi ni vitu viwili tofauti.
Mhe. Jafo amesema wataalamu walisema shule ya sekondari ina nafuu lakini amesema hapana lazima sekondari Karatu ifanyiwe ukarabati. Amesema nataka iwe shule ya karatu iongoze kwa unadhifu na ubora wa majengo. Amesema uwekezaji katika elimu ndio unasababisha kiwango cha ufaulu kuongezeka sanaa. Amesema Karatu sekondari inakabiliwa pia na uhaba wa mabweni, amesema atatuma wataalamu kutoka Tamisemi ili wafanye tathimini ya kina ya majengo.
Mhe. Jafo ameahidi fedha za haraka za mwanzo kiasi cha million 70 kwa ajili ya ujenzi wa bweni moja wiki ijayo. Amesema bweni hilo litajengwa kwa force acoount ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya karatu kuanza kazi ya ujenzi wa bweni jumatano, amesema anataka kazi ya ujenzi wa bweni ikamilike ndani ya miezi miwili.
Mhe. Jafo amesema Karatu sekondari inafanya vizuri kitaaluma, lakini amesema wanauwezo mkubwa wa kufanya vizuri zaidi. Amesema anatamani sana kuhudhuria mahafali ya mwaka huu ya shule ya sekondari Karatu sekondari. Amesema shauku yake ni kuona kila mtu Tanzania pindi matokeo ya kidato cha nne yanapotoka atamani mtoto wake kwenda Karatu sekondari.
Mhe. Selemani Jafo katikati akiwa anatembelea eneo la shule ya sekondari Karatu.
Amewataka wanafunzi wa kidato cha tano na sita kuazimia kwamba hakuna zero, ametaka vijana kupambana kwa heshima ya Karatu sekondari. Ametaka vijana hao kuhakikisha Karatu sekondari kuwa katika shule 50 bora Tanzania katika ufaulu wa matokeo ya kidato cha sita.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa