Maadhimisho ya kilele ya siku ya utalii yamefanyika wilayani Karatu yakijumuisha shughuli mbalimbali za utunzaji wa mazingira. Halmashauri ya wilaya ya Karatu kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi wamehamasisha waananchi kutunza mazingira katika kilele cha siku ya utalii duniani.
Kaimu mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Iddi Kimanta amesema mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha kuwepo kwa mvua nyingi kwa kipindi kifupi na kiangazi kirefu. Amesema mabadiliko ya nchi yamesababisha kuwe na upungufu wa maji kwenye maeneo mbalimbali, kuongezeka kwa mmonyoko wa ardhi, maeneo ya wachungaji kumekuwa na upungufu wa malisho.
Mhe. Kimanta amesema shughuli zetu za kibinadamu zenye manufaa ya muda mfupi zinaathari kubwa kwa mazingira. Amesema shughuli za kukataa miti kwa shughuli mbalimbali; kuchimba mchanga kwa ajili ya kujengea, tunaongeza mifugo kwa ajili kuongeza uchumi inayosababisha uhaba wa malisho na uharibifu wa ardhi. Mhe .Kimanta amesema, “kama mazingira yetu tutayaharibu hata maisha yetu tutayaharibu.” Amesema kuna bango limeonyeshwa na watoto, linasema, “ukipenda mazingira umependa maisha yako. “ uharibifu wa mazingira unaoendelea hivi sasa unabadilisha hali ya hewa.
Mhe. Kimanta amesema kuna bango jingine la watoto linasema, “ukiona mtu amekaa kwenye kivuli cha mti ujue mti huo kuna mtu aliupanda.” Amesema ili tuendelee kuitunza dunia tunahitaji kupanda miti. Uharibifu wa mazingira unaatahari kubwa katika shughuli za utalii ni jukumu letu kuandaa hali ya uchumi wa nchi yetu hapo baadae. Mhe. Kimanta ametoa wito kwa wananchi kutunza vyanzo vya maji, kupanda miti, na kutunza mazingira kwa namna wataalam watakavyotushauri.
Mhe. Iddi KImanta kaimu mkuu wa wilaya ya Karatu, akikata utape kama ishara ya kuzindua kampeni ya kupanda miti ( Birthday Tree Plant )
Naye Brother John sulle Mkurugenzi wa (TAJPI) The a-aray justice and peace initiative amesema, tumezindua mpango wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa kupanda miti (Birthday Tree Planting) Ameongeza kusema tumeamua kuunganisha siku ya utalii na mazingira kwa sababu bila hali nzuri ya mazingira, utalii hauwezi kufanikiwa.
Brother Sulle amesema Tajpi inahamasisha kupanda miti wakati wa kuadhimisha siku zetu za kuzaliwa. Amesema tumeunganisha siku ya utalii na mazingira kwa kutumia kauli mbiu ya Utalli na Hali bora ya Maisha na kauli mbiu ya mazingira Tunza Ardhi, Ardhi Ikutunze Wewe.
Bi, Rehema Peter katibu mkuu wa Tajip amesema global climate srtrike vuguvugu la mabadiliko ya tabia ya nchi, limeleenga kukemea swala zima la mabadiliko ya tabia nchi. Bi Rehema amesema vuguvugu limelenga watu wote lakini hasa kizazi kipya, ambao jukumu lao kubwa ni kupaza sauti kukemea swala la mabadiliko ya mazingira, swala la mabadiliko ya nchi, kuzuia uzalishaji na matumizi ya gesi ya ukaa. Bi rehema amesema tumesherekea siku ya utalii duniani ili tuchukue hatua juu ya maswala ya uwindaji haramu, na kuzuia sumu mbalimbali zinazotumika kwenye viwatilifu mashambani. Amesema maadhimisho hayo yamefanyika ili yawe chachu kwa jamii nzima, kupinga maswala yote yanayosababisha uharibifu wa mazingira na masawala yote yanayohusika na kuumiza na kuathiri, Mama Ardhi.
Bi Rehema, amesema shughuli za mazingira na utalii ni watoto mapacha, kama hakuna mazingira salama kwa viumbe hai utalii unaathirika. Amesema shirika la tajip linajenga uelewa kwa jamii, hasara na faida za kutunza mazingira lakini faida zinazotokana na utalii. Tunachukua hatua kwa kaya duni kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali na kugawa miti ili waoteshe kwenye famila. Tajip imefanya hamasa ya kupanda miti kupitia serikali za vijiji na shule, Bi Rehema ametoa wito kwa taasisi nyingine kuunga mkono juu ya uhifadhi wa mazingira ili utalii uwe endelevu.
Naye Christina Joseph mwanafunzi wa Tumaini ameomba serikali kuweka kipaombele katika usafi wa mazingira. Amesema wanaungana na watoto wote dunia katika vuguvugu la mabadiliko ya tabia ya nchi. Ameomba jamii kufanyia kazi ujumbe uliotolewa katika maadhimisho ya siku ya utalii yalioenda sambamba na shughuli za uhifadhi wa mazingira.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa