Na Tegemeo Kastus
Kikao cha wadau wa afya na watu binafsi (PPP) kimetoa elimu juu ya ugonjwa wa virusi vya corana (COVID-19) kwa watu wenye Hotel wilayani Karatu. Kikao hicho kimepata mwitikio mkubwa na kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo.
Mhe. Mahongo amesema hakuna mgonjwa aliyegundulika mwenye virusi vya corona wilayani Karatu. Amesema uelimishaji umeanzia kwa watu wa Hotel, kwa sababu wanakutana na watu wengi wa nje. Uelimishaji umelenga kupata uelewa juu ya corona (COVID-19) ikoje mtu mwenye dalili yukoje. Amesema elimu itasaidia watu hotel kutoa taarifa endapo watamuona mtu mwenye dalili, ili hatua ziweze kuchukuliwa. Mhe. Mahongo amesema uelimishaji utaendelea kwa makundi mengine ili wananchi waweze kupata elimu ya ufahamu na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa virusi vya corona.Mhe. Mahongo amesisitiza hakuna taarifa ya kukataza shughuli yeyote kutofanyika, watu waendelee na kazi kama kawaida.
Mhe. Mahongo ameomba watu wenye Hotel watoke wakiwa wanajua wamepata mafunzo ya kujiandaa, iwapo itatokea tumepata mtu mwenye dalili za mgonjwa wa Corona (COVID-19) waweze kutoa taarifa. Amesema moja ya viashiria vya virusi vya corona ni mafua, amehimiza watu kutoa taarifa kwa wataalamu ili wachukue sampuli ya vipimo na kuthibitisha. Amesema taarifa zote zitafuatiliwa; Mkuu wa wilaya ametoa namba yake ya simu ya mkononi, namba ya Mganga mkuu, namba ya Afisa Afya wa wilaya namba ya Mratibu wa magonjwa ya mlipuko (epidemolojia).
Mhe. Mahongo ameomba watu wasije wakapotosha elimu hiyo, kikao kililenga kupeana maarifa na watu kuwa na utayari. Amesema wametenga hospitali ya wilaya Karatu Lutherani na kituo cha Afya ya Fame kwa ajili ya kuwekea karantini. Mhe. Mahongo amehimiza watu watumie maji safi yanayotirirka na sabuni pamoja na sanitizer.
wadau wa maswala ya afya na watu binafsi wakisikilza makini wakati wa kikao.
Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Mustafa Waziri amesema lazima watu wa Hotel wawe na (Mask) kwa tahadhari ya virusi vya corona (COVID-19) endapo mgonjwa akitokea. Amesema (mask) zinauzwa 132000 kwa mask 20 package, Dkt. Waziri amesema Mask zinauzwa MSD. Mganga mkuu amesema kuna sheria inayoelekeza kuwa na vifaa vya tahadhari amesema baada ya muda wa kutekeleza maelekezo ya vifaa kupita atafanya ukaguzi kwenye hotel akikuta vifaa hivyo hakuna atafunga Hotel.
Mganga mkuu Dkt. Waziri amesema lazima ofisi za serikali na Mahoteli ziwe na sehemu ya kuoshea mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni. Amesema mgeni anapoingia Hotelin au anapotoka anawe mikono na atumie sanitizer. Dkt. Waziri ameomba watu kuepuka salamu ya kushikana viganja vya mikono na badala yake watu wasalimiane bila kushikana.
Mratibu anayehusika na magonjwa ya Mlipuko kituo cha afya Karatu Robert Hongo amesema kwamba kuna aina 30 za virusi vya corona lakini kwa ufatfiti uliofanyika wa kisayansi ni aina 7 za virusi zinazoweza kuleta madhara kwa binadamu na mnyama.
Ndugu. Hongo amesema mgonjwa huanza kuwa na mafua ya kawaida na huendelea mpaka kuwa na mafua makali. Amesema maambukizi yanaenea hasa pale mtu aliyeathirika anapoongea na mtu mwingine ambaye hajaathrika, anasema kwa kuongea mtu aliyeathrika wakati wa kuongea kuna zile chechembe za maji zinazoruka kuelekea kwa msikilizaji, Ndugu. Hongo anasema chembechembe zikimfikia mtu ambaye hajaathrika zinaweza kumletea ugonjwa.
Ndugu. Hongo anasema virusi wa corona hawakai zaidi ya masaa mawili kwenye mazingira. amesema mtu aliyeathirika anaweza akasambaza virus kwa njia ya kupenga makamasi, anasema pia mtu mwenye ugojwa anaweza kusambaza virusi kwenye mazingira kwa njia ya kupiga chafya. Mtu anaweza kuathirika kwa kuzungumza na mtu aliyeathirika na virusi vya corona wakati wa kuongea kutokana na ile hali ya kubadilishana hewa. Dkt. Hongo anasema virusi vya corona vinaweza kusambaa kwa njia ya kugusa sehemu ambayo muathirika amepenga kamasi akashika mlango, na wewe ukapita ukagusa ndani ya yale masaa mawili na kupeleka mkono maeneo ya uso.
Ndugu. Hongo amesema si waathirika wote wa ugonjwa wa virusi vya corona watakuwa na dalili zote zinazofanana, amesema dalili za mwanzo ni pamoja na kuwa na homa, mgonjwa anakuwa na uchovu na kikohozi kikavu. Misuli ya mwili kukaza mafua kutiririka, maumivu ya koo na baadhi ya wagonjwa wengine kuharisha. Ndugu. Hongo amesema sio wote wataambukizwa wataonesha dalili hizi, hii hutegemeana na kinga ya mwili ya mhusika.
wadau wa maswala ya afya na watu binafsi wakifuatilia utoaji wa mada kwa umakini
Ndugu . Hongo amesema wameshatoa elimu kwa wataalamu wa afya katika vituo vyote vya afya amesema si kila mafua ni virusi vya corona. Amesema mafua yanasababishwa na vitu vingi ni vyema mtu akaenda kituo cha afya ili wataalamu wamsaidie kutofautisha mafua ya kawaida na mafua yenye virusi vya corona.
Ndugu. Hongo amesema unapohisi umegusa vitu ambavyo si salama nawa kwa maji safi, salama yanayotitririka na tumia sanitizer. Ndugu. Hongo amesema epuka kugusa pua midomo na kaa mbali na mtu mwenye mafua au kikohozi. Amesema unaweza ukapata maambukizi leo kulingana na kinga yako ukaonesha dalili siku ya 14 ndio maana tunajengeana uwezo wa uelewa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa