Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amefanya ziara katika kata ya Kansay na kutembelea zahanati ya Ng’aibara na Zahanati ya Laja. Amekagua miundo mbinu ya zahanati hizo, pamoja na kuangalia, hali ya upatikanaji wa dawa katika zahanati hizo. zahanati ya Ng'aibara inatarajiwa kufanyiwa ukarabati wa majengo katika kipindi cha mwaka huu wa fedha unaonza sasa.
Mhe. Theresia amemuomba mwenyekiti wa kijiji cha Ng'aibara kutumia vizuri fedha walizopewa na Global fund ili zinufaishe wananchi waliolengwa. Amesema zahanati hiyo ikiboreshwa wagonjwa watakuwa wakipata rufaa wanakwenda hospitali ya wilaya. Amewapongeza wananchi kwa kujenga jengo lenye ubora ambalo bado halijamalizika kupauliwa. Mhe. Theresia amesema mfumo wa kuomba dawa umebadilika kila kituo kinaandika mahitaji ya dawa inazohitaji kwenye kituo hivyo ni vyema kituo kikaagiza dawa kulingana na Mahitaji ya kituo. Amesema bajeti ya afya ilikuwa billion 36 kipindi cha nyuma lakini sasa hivi bajeti ya afya imeongezeka na imefikia takribani billion 270 kwa mwaka. Kituo hicho awali kilipata nyota sifuri kwa kuwa na huduma duni. Lakini sasa mabadiliko makubwa yamefanyika katika zahanati ya Ng’aibara ikiwa ni pamoja na kuweka daktari mmoja na muuguzi.
Mkuu wa wilaya akikagua jengo la watumishi zahanati ya Ng'aibara
Mganga mkuu wa wilaya Mustafa Waziri amesema kituo hicho cha Ng’aibara kimepewa kiasi cha 154,208,000. Fedha hizo 25 % zitatumika kulipa mafundi na iliyobakia ni kwa kujenga miundo mbinu na kukarabati zahanati hiyo. Shughuli hizo za ukarabati wa kituo cha afya zinahusisha; ujenzi wa vyoo, nyumba ya mtumishi, kuweka uzio wa wavu, na ujenzi wa maabara. Lakini pia kuweka umeme katika kituo hicho na kujenga na kuweka miundo mbinu ya maji.
Dkt. Mustafa amesema changamoto ya zahanati hiyo ni watu kutopenda kuhudhuria na kupata huduma za afya katika kituo vya afya. Ametoa rai kwa wakinamama wajawazito kwenda kujifungulia katika vituo vya afya. Karatu ina 47% ya wakinamama wanaojifungulia katika vituo vya afya kati ya 60% inayotakiwa na serikali. Ameomba pia wajumbe wa kituo hicho kuhamasisha watu kupata bima ya afya iliyoboreshwa ambayo ni shilingi 30000 watu sita kwa kaya. Ambayo na serikali nayo inatoa fedha kiasi cha 30000 kwa kila aiyechangia mfuko wa bima ya afya. Dkt. Mustafa amesema bima ya afya inasaidia hospitali kuongeza uwezo wa kupata dawa kadri ya mahitaji ya kituo husika.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa