Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, Mhe. Jubilate Gerson Mnyenye ameongoza kikao cha pili cha baraza la madiwani kilichofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri. Katika kikao hicho mihutasari ya vikao vya tarehe 27 na 28 april ilisoma na kuthibitishwa.
Kikao hicho kilimchagua Mhe.Lazaro Simoni Bajuta Diwani wa kata ya Ganako kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye alipata kura 12 kati ya 19 na kura 7 alipata mpinzani wake Mhe. Lazaro Emanuel Gege Diwani wa Mang’ola. Pia wajumbe wa kamati ya Elimu Afya na Maji walimchagua Mhe. John Lucian Mahu, Diwani wa Endamarariek kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo,wajumbe wa kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira na ikamchagua Mhe. Josephat Martin Margwe Diwani kata ya Oldeani kuwa mwenyekiti wa kamti hiyo.
Katika kikao hicho taarifa ya Kamati ya Kudhibiti Ukimwi, kamati ya Elimu Afya na Maji, kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingirana kamati ya Fedha Uongozi na Mipango zilipokelewa.
Mhe. John Lucian Mahu, mwenyekiti wa kamati Elimu ya Afya na Maji alisema kuna mpango wa kuziandikia barua ya kuzipongeza shule zilizofanya vizuri mitihani ya Taifa na kuziandikia barua ya kujieleza kwa shule zilizofanya vibaya. Pamoja na hilo kamati yake inataka umeme ufike sehemu zote zenye vyanzo vya maji ili kupunguza gharama za maji. Mhe. John alisema kamati yake pia ina pambana na madada poa katika mji mdogo wa Karatu na imefanikiwa kukamata wakina dada 23 ambao kati yao 2 ni wanafunzi wa sekondari Welwel. Alisema tatizo linalosumbua zoezi hilo ni wazazi ambao hutetea watoto wao kwamba hawana tabia hizo.
Mhe Willy Qambaro Mbunge wa Karatu ambaye lichangia katika kamati hiyo aliomba Mkurgenzi Mtendaji kusambaza walimu wa kike katika shule za pembezoni iliwaweze kuwasaidia watoto wa kike katika shule hizo ambazo nyingi zina walimu wa kiume peke yake. Kamati hiyo pia iliomba Wenyeviti wa vijiji, Watendaji wakishirikiana na Madiwani wawahimize wazazi watoe chakula ili wanafunzi wapate chakula wakiwa shuleni.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa