Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe Dadi Horice Kolimba amesema ndani ya miaka 61 ma Raisi wa Tanzania wamelifungua Taifa hususani katika Uchumi na Nidhamu Tangu Tanzania ipate uhuru chini ya Muasisi Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere hadi uongozi wa Awamu ya (6) chini ya Mhe Raisi Samia Suluhu Hassani.
Mhe Kolimba ameeleza hayo wakati akifungua mdahalo wa miaka 61 ya uhuru uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu kuzungumzia maendeleo ya wilaya ya Karatu ndani ya miaka 61 ya Uhuru nakusema kuwa katika kipindi cha uongozi wa awamu ya sita Mhe Raisi Mama Samia Suluhu Hassani amesimamia matumizi ya fedha kuanzia ngazi taifa hadi wilaya ikiwemo mfumo wa "Force Account" ambao umesaidia ujenzi wa miundo mbinu mikubwa na ya kihistoria pamoja na kuboresha huduma za jamii Afya,Maji,Elimu, na Barabara.
Kwa wilaya ya Karatu haikuwahi kuwa na hosipitali ya wilaya lakini ndani ya miaka 61 ya Uhuru tayari kuna Hosipitali kubwa na ya kisasa ya Wilaya inayo tarajia kuhudumia watu 290,000 pia serikali imetoa fedha kiasi cha Bilioni 480 kwaajili ya ujenzi wa madarasa vile vile ndani ya miaka 61 ya uhuru wilaya ya Karatu sasa ina chombo kimoja cha kusimamia huduma ya Maji (KARUWASA).
Aidha Mhe Dadi Horis Kolimba ameongeza kuwa miaka 61 ya uhuru sasa Karatu ina miundombinu ya kisasa ya barabara na bado kazi inaendelea.
Katika mdahalo huu wa miaka 61 ya uhuru wataalamu, wakuuu waidara wazee walio kuwepo wakati nchi ikipata uhuru wamezungumzia kazi kubwa iliyo anzishwa na Muasisi wa Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere na inaendelea hadi uongozi wa awamu ya Sita chini ya Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan.
James Emmanuel mwakilishi wa vijana wilaya ya karatu katika Kongamono hili ameeleza kuwa miaka 61 ya uhuru wilaya ya Karatu fursa za kiuchumi zimefunguka katika Utalii pamoja na mkopo unaotolewa na Halmashauri wa 4% umemnufaisha binafsi kwani kwasasa wameweza kufungua kiwanda cha usindikaji wa mikate wilayani Karatu na kutoa unafuu wa Maisha.
Kwa upande wake afisa Elimu Msingi wilaya ya Karatu ameeleza kuwa katika miaka 61 ya Uhuru wilaya ya Karatu ina Shule 110 za msingi na 9 ambazo sio za serikali na ndani ya miaka 61 ya uhuru wilaya ya Karatu ina wanafunzi 60072 ikiashiria kuwa wanafunzi wengi wana pata elimu kutokana mpango wa serikali wa elimu bila malipo.
Afisa elimu sekondari wilayani Karatu ameeleza kuwa kuna shule 35 za sekondari na ndani ya Miaka 61 ya uhuru kuna wanafunzi 12907 wa Sekondari wilayani Karatu ,nakueleza kuwa kwa sasa serikali inajenga shule zingine 2 ambazo mwakani zitakamilika na kufanya wilaya ya Karatu kuwa na shule 37 za sekondari na kwasasa kuna upungufu wa walimu.
Mwl Marko Aney mkuu wa shule ya sekondari Karatu ambayo ni shule pekee iliyo kuwepo Karatu baada ya kupatikana uhuru ameeleza kuwa ndani ya miaka 61 ya Uhuru ujinga na giza limeondoka na kuwa viongozi wote wa Tanzania wametoka kwa Mungu na ata awamu ya 6 shule ya Karatu sekondari imepewa milioni 700 kuboresha shule hiyo na kazi imekamilika 100%.
Kwa upande wa Afya Mganga mkuu wa Wilaya Dr Lucas J. Kazingo ameeleza kuwa wakati wa uhuru magonjwa yalikuwa mengi na yametokomezwa mfano polio iliyo tokomezaa mwaka 1976.
Kazingo ameongeza kuwa ndani ya miaka 61 ya uhuru wakati wilaya ya Karatu inaanzishwa mwaka 2000 kulikuwa na vituo vya kutolea huduma 10 na sasa kuna vituo vya kutolewa huduma 66 na zahanati 53 na Mpaka sasa bilioni 5 zimetolewa na serikali kwaajili ya kuboresha vituo vya afya na kwa sasa kuna asilimia 99% upatikanaji wa dawa na vifaa tiba wilayani Karatu.
Salum Abdul kalymonda afisa rasilimali watu wa wilaya ya Karatu ameeleza kuwa ndani ya miaka 61 ya uhuru kuna mafanikio makubwa katika kusimamia haki kwa mwajiri na mwajiriwa mpaka mahakama ya rufaa ikiwa ni pamoja na kuongezeka rasilimali watu kuhudumia umma wa Tanzania kwaa wakati na kwa uhakika katika kila idara na wilaya ya Karatu imeendelea kutoa huduma bora na kwa ubora unaotakiwa kwa wananchi wa kada na ngazi zote katika dhana ya upeo wa utawala bora na umakini katika kuzingatia sheria za kazi na wajibu kwa kila mtumishi ikiwemo uwajibikaji , udhibiti wa rushwa hadi ngazi ya vijiji, haya ni mafanikio makubwa ya uhuru ndani ya miaka 61 ya uhuru kwa wilaya ya Karatu.
Cp leberatus Kazungu mkuu wa idara ya Fedha wilaya ya Karatu ameeleza kuwa ndani ya miaka 61 ya Uhuru kumekuwa na wahasibu wengi na ukuaji wa Tehama ambao umerahisisha utendeji na kuthibiti ufujaji wa mapato kutokana na uwepo wa "POS MACHINE" yenye udhibiti mkubwa na uratibu mzuri wa taarifa Za kifedha kwa kila Fedha ya umma Ndani ya wilaya ya Karatu na Taifa kwa ujumla.
Aidha Kazungu ameeleza kuwa 40% ya mapato ya Halmashauri yameboresha huduma za jamii ikiwemo miradi ya Afya,Elimu,Maji na MiundoMbinu ikiwo ujenzi wa barabara zenye hadhi na imehamasisha wananchi kuchangia maendeleo.
Ibrahimu Lymo kaimu afisa kilimo Mifugo na Uvuvi ameeleza kuwa ndani ya miaka 61 ya Uhuru wilayani Karatu kumekuwa na maboresho makubwa ikiwemo idadi ya watumishi walikuwa 6 na sasa kila kata kata zote 14 kuna afisa ugani , na wataalamu wa mifugo na uvuvi (uvuvi ziwa Eyasi), upatikanaji wa chanjo za mifugo kwa uhakika na usimamizi thabiti wa punguzo na unafuu wa huduma za ugani ikiwemo punguzo la Mbolea lililotolewa na serikali kufikia walengwa pamoja uhimilishaji wa mifugo miongoni mwa mafanikio makubwa ndani ya miaka 61 ya uhuru wilayani Karatu.
Lemunge utouh Afisa Tehama wa halmashauri ya Wilaya ya Karatu ameeleza kuwa kwa Miaka 61 ya Uhuru huduma za kifedha kutuma na kupokea fedha zimeboreshwa, huduma za mawasiliano ya simu wilayani Karatu zimboreshwa kila Kijiji, matumizi ya Tehama kwenye taasisi za serikali ikiwemo Elimu ,Afya ,ukusamyaji wa mapato miongoni mwa Nyingi zimeboreshwa na serikali imetoa vishkwambi 20 kwaajili ya vikao vya baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Karatu jambo ambalo limepunguza matumizi ya makabrasha.
Godfrey Edward afisa biashara wa Halmashauri ya karatu ameeleza kuwa miaka 61 ya Uhuru utoaji wa leseni sasa unafanyika chini ya halmashauri na kutumia mifumo wa Tehama jambo ambalo limeondoa ubadhilifu wa fedha za Umma , na katika miaka 61 ya Uhuru imeanzishwa idara ya viwanda biashara na uwekezaji haya yamekuwa mafanikio makubwa
Aidha bwana Godfrey ameongeza kuwa ndani ya miaka 61 ya uhuru mapato yameongezeka kufikia Tsh milioni 722,551,724.84 kwa wilaya ya Karatu na kazi inaendelea.
Salome kivuyo Afisa utalii ameeleza kuwa pamoja na idara yake kuwa inauza "Raha" kwa sasa kuna hoteli za kitalii 71 na ajira zaidi ya 300 zimepatikana kutokana na Kukua na usimamizi thabiti wa serikali katika sekta ya utalii Royal Tour miongoni mwa maboresho makubwa ya kisekta wilayani Karatu na kwasasa zaidi ya wageni laki Nne wanapita wilaya ya Karatu kuelekea Ngorongoro na Serengeti na wageni elfu kumi na Tatu wanatembelea wilaya ya Karatu kwaajili ya utalii wa kitamaduni ziwa Eyasi mapato yameongezeka kupitia ushuru "service Levy"na Michango ya maendeleo ya kutembelea hifadhi na vivutio vya Utalii wilayani Karatu ndani ya miaka 61 ya Uhuru sekta ya Utalii imekuza uwekezaji haya ni mafanikio Makubwa.
Bi Kivuyo ameeleza kuwa Baada ya Uhuru halmashauri ya wilaya ya Karatu imetambuliwa na shirika la kimataifa la "Unesco" kuwa na hadhi ya Ki Geolojia katika historia ya dunia kwa vizazi vyote jambo ambalo nimafanikio makubwa ndani ya miaka 61 ya uhuru.
Walter Nnko Afisa maendeleo ya Jamii ameeleza kuwa "ndani ya miaka 61 ya uhuru mikopo ya halmashauri sasa inatolewa bila riba haya ni mafanikio makubwa"
Bwana Walter ameeleza kuwa katika miaka 61 ya uhuru kuna maboresho makubwa kupitia TASAF na katika uongozi wa awamu ya 6 walengwa wa TASAF Awamu ya tatu wamepewa fedha zaidi ya shilingi bilioni 10 hii imetanua wigo wa makundi ya kijamii wilayani Karatu kujiajiri na kufungua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
Dismas Ngole Afisa ardhi wilaya ya Karatu ameeleza kuwa katika miaka 61 ya uhuru upatikanaji wa ardhi hauna ubaguzi na halmashauri Ya Wilaya ya Karatu imefanikiwa kupima viwanja 6017 na vipo kwenye mfumo wa ki Electroniki,na usimamizi wa anunwani za makazi 58951 kwa wilaya ya Karatu haya yamekuwa mafanikio makubwa Ikiwemo upatikanaji wa fursa za vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi na utoaji wa haki za ardhi na utoaji wa tozo za ardhi za kielectroniki ni miongoni mwa mambo makubwa yanayoendelea kufanyika ndani ya miaka 61 ya Uhuru.
Muhandisi Henry Chao Meneja wa Shirika la Umeme nchini TANESCO kwa Wilaya ya Karatu ameeleza kuwa kwa sasa kuna vijiji 3 tu vimesalia kupata umeme na maeneo hayo tayari kazi inaendelea tayari transfoma nguzo na utandazaji wa nyaya una endelea kwa sasa katika vijiji hivyo na mpaka june 2023 kazi hizi zitakuwa zimekamilika kila mwananchi wa wilaya ya Karatu anafurahia utendaji thabiti wa watumishi wa umma katika miradi yay maendeleo haya ni mafanikio makubwa ndani ya miaka 61 ya Uhuru.
Muhandisi Mbaraka Mahamudu Kilangai Meneja wa Ruwasa ameeleza kuwa ndani ya miaka 61 vijijini huduma ya maji inapatikana kwa 72% na kwa sasa kuna miradi ya shilingi bilioni 2.4 za Kitanzania itakayo fikisha upatikanaji wa maji kufika zaidi ya 85% vijijini watakuwa wanapa huduma ya maji safi na salama hizi zikiwa ni juhudi Kubwa za viongozi wa taifa hili kuweka wananchi kipaombele kupata huduma ikiwemo kumtua mama ndoo Kichwani.
Mkurugenzi wa mamlaka ya usambazaji wa maji Karatu (Karuwasa) Ndg. Stephen J. Siayi ameeleza kuwa ndani ya miaka 61 ya Uhuru bei ya maji kwa wilaya ya Karatu imepungua toka shilingi 3500 hadi Tsh 1300 na Tsh 1000 kwa Dp za umma na kwa sasa huduma za maji zimeboreshwa kuna visima vya maji 13 na vyanzo vya mito 2 vinavyo zalisha lita 6,051,600 kwa siku na huduma ya maji safi na salama inapatikana kwa uhakika na kwa wakati ndani ya wilaya ya Karatu hii ni dhana ya uwajibikaji na uongozi bora ndani ya Miaka 61 ya Uhuru katika kuwahudumia wananchi kuanzia ndani ya wizara ya maji mpaka mamlaka za maji ikiwemo Karuwasa iliyo anza kazi ndani ya Muda mfupi kwa kasi na ubora wa kuchapiwa mfano na mamlaka zingine za maji nchini.
Bwana Siay ameongeza kuwa kwa sasa usajili wa wateja wa huduma ya Maji wilayani Karatu wateja 4636 wamesajiliwa kwenye mfumo wa Tehama wa ( Unified Biling system) (eGA Maji is) na kazi ya usajili imefikia 90% kwa sasa na Karuwasa 2021/2022 kupitia mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWASA) na Kwa kutumia "force Account" Karuwasa imepokea fedha jumla ya Tsh 490,337,644.05 kutoka katika fedha za "UVICO" kuongeza mtandao wa usambazaji maji Wilayani Karatu " haya yamekuwa mafanikio makubwa ndani ya miaka 61 ya uhuru" amesema Bw. Stephene J Siay Mkurugenzi wa Karuwasa.
Muhandisi Msetu Naide Madara meneja wa Tarura Wilaya ya Karatu ameeleza kuwa katika miaka 61 ya uhuru Wilaya ya Karatu ina Kilometa 45.945 za lami yaani km1.945 ndani ya Mji wa Karatu na km 44 barabara kuu kwenda Ngorongoro , barabara za changarawe ni km 153.05 na barabara za udongo ni km 557.035 za mtandao wote wa barabara Wilayani Karatu.
Madara ameeleza kuwa Kabla ya Uhuru ndani ya Wilaya ya Karatu Kulikuwa na vivuko vinne (4) tu na sasa katika miaka 61 ya Uhuru kuna vivuko 397 ikiwa ni madaraja 42 ,makalvati 299 na Madrifti 56 na mikakati ya serikali nikuweka taa kila panapo wekwa lami ndani ya Wilaya ya Karatu na kwa sasa maeneo Mengi yanapitika kwa vipindi vyote vya mwaka.
Mwenyekiti wa Baraza la wazee Charles Goranga amesema kuwa tayari baraza la wazee Wilaya ya Karatu limeshapata fedha kwa ajili ya kujenga mnara wa Kumbukumbu ya Uhuru bazo ni zaidi ya Tsh milioni Tano (5,000,000) ambapo kutakuwa na sehemu ya Maktaba kwa ajili ya kuweka KUMBUKUMBU za waasisi wa Taifa pamoja na wazee waliokuwepo wakati wa Uhuru Wa Wilayani Karatu na waasisi wa Uhuru wa Tanzania dhumuni niku uhifadhi ukweli kuwa historia haidanganyi ndani ya miaka 61 ya Uhuru ni mambo makubwa yalianzishwa na waasisi wa taifa na yanaendelea kuenziwa na itakuwa ni ubunifu wa eneo la ukusanyaji wa mapato ndani ya Wilaya Ya Karatu kwani itavutia utalii.
John Zakaria Tipe Makamu Mwenyekiti wa baraza la wazee Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karatu ameeleza kuwa mafanikio yote yanayo onekana ndani ya Miaka 61 ya uhuru ni misingi imara iliyo wekwa na Chama Cha Mapinduzi ikiwemo kutoa eneo la kujenga ofisi za serikali ilipo halmashauri ya wilaya ya Karatu na taasisi nyingine za serikali haya yote ameshuhudia na kusimamia ndani ya Miaka 61 ya Uhuru.
Akihitimisha mdahalo huu wa miaka 61 ya uhuru mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe Dadi Horice Kolimba ametoa shukurani kwa wote walio changia mdahalo wa miaka 61 ya Uhuru na kueleza kuwa wilaya itaendelea kuandaa makongamano kama haya ili kuongeza dhamira ya kujenga uzoefu zaidi kwa vijana na vizazi hadi vizazi kuongeza juhudi na maarifa kulipeleka taifa letu mbele na kwa kasi zaidi pasina kusahau kuifahamu historia ya nchi ya Tanzania kudumisha amani utulivu uwajibikaji utawala bora na uchapa kazi.
Mhe Kolimba ameeleza kuwa nimafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo na kutoa wito kwa wananchi kushiriki katika miradi ya maendeleo na kuitunza miradi ya maendeleo inayo letwa na serikali.
Kauli mbiu ( Miaka 61 ya Uhuru Amani na Umoja ni nguzo ya maendeleo yetu).
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa