NA TEGEMEO KASTUS
Maendeleo yeyote katika nchi yanapangwa kutokana na takwimu za watu, serikali inajenga miundo mbinu ya maendeleo kutokana na takwimu ya idadi ya watu. Takwimu ndio inasaidia kujua mahitaji ya watu kulingana na umri. Hivyo kujua idadi sahihi ya wakazi inarahisha katika kupanga mikakati endelevu ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kutengeneza sera zinazoendana na mahitaji ya jamiii.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa anafungua mafunzo ya siku tatu ya kuandaa watendaji watakao shiriki katika zoezi la kusajili watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. Usajili wa uandikishaji wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano unafanywa na RITA kwa kushirikiana na shirika la UNICEF na zoezi hili lilianza nchini Tanzania tangu mwaka 2013. Usajili huo unatarajiwa kufanyika kwa muda wa siki 90, Mh. Kayanda ametoa rai kwa watendaji kufanya zoezi hilo kwa ukamilifu wake. Amesema kazi ifanyike kulingana na maelekezo ya wataalamu.
Mh. Abbas Kayanda (kulia) akizungumza na watendaji wakati wa ufunguzi wa mafunzo
Mh. Kayanda amesema serikali inataka kuwa mpango taarifa wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, amesema katika wilaya ya Karatu watoto zaidi ya 40259 wanatarajiwa kusajiliwa. Amesema kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano anapaswa kusajiliwa, Amesema kwa watoto wa chini ya miaka mitatu tunatarjia kushirikiana na wasimamizi wa vituo vya afya kupata takwimu za watoto wanaokuja kupata huduma za chanjo. Amesema kwa watoto walio juu ya umri wa miaka mitatu na mitano watendaji ndio watakuwa na jukumu la kupita katika maeneo yao ya kiutendaji ili kuhamashisha wazazi wawasajili watoto.
Amesema takwimu hizo zitasadia serikali katika mpango wake wa elimu bure lakini katika matibabu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Mh. Kayanda amesema ni vyema watendaji wa zoezi hilo waheshimu viapo watakavyoapa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa ufunguzi wa semina
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa