Afisa elimu sekondari amepongeza shule za sekondari za kidato cha tano na sita kwa matokeo mazuri waliyopata katika mitihani yao ya taifa. Matokeo hayo yanaashiria kuna jitihada madhubuti za kuinua taaluma zinafanyika katika shule hizo. Amesema hayo katika ziara ya kutembelea shule za sekondari kujionea utendaji kazi wa walimu juu ya maelekezo aliyowapatia.
Bi, Kalista Maina amesema ziara hizo ndio kwanza zimeanza, lazima Karatu tusogee mbele kupitia mikakati tuliojiwekea. Amesema amefurahi kuona shule ya sekondari Karatu haina ufaulu wa daraja sifuri kuwa na wanafunzi zaidi ya 200 ni jambo la kipekee. Amesema shule kama Ganako sekondari wameishia ufaulu wa daraja la tatu hakuna daraja la nne wala daraja sifuri. Amesema Anagamazo nao wamefanya vizuri na matokeo yanatoa mwelekeo wa njia tunayopaswa kuifuata. Bi, Maina amesema hao wameshaanza kujitambua, sasa ni wakati wa kidato cha nne nao kufuata mwelekea huo.
afisa elimu sekondari akiwa katika ukaguzi wa utendaji kazi wa walimu
Bi. Maina amesema alihudhuria mahafali ya shule ya Agamazo akawapa Mikakati ya mbinu 25 za kutumia ili kuinua ufaulu wa kitaaluma. Amesema wameipokea vizuri na wanaifanyia kazi, kwa sababu nimeona mwelekeo wa matokeo yao. Ameongeza kusema mikakati aliyotoa, kwa mwalimu mfuatiliaji lazima atapata matokeo chanya.
Afisa elimu taalumu Ndugu Robert Sijaona amesema matokeo ya kidato cha sita ufaulu wa kitaaluma umepanda. Amesema hiyo inatokana na mipango ya idara ya elimu iliyopanga katika kuinua kiwango cha taaluma. Amesema kwa Karatu sekondari kuna wanafunzi waliopata daraja la kwanza 91 wanafunzi waliopata daraja la pili 170 na daraja la tatu 99 na wanafunzi waliopata daraja la nne wako 10. Amesema Ganako sekondari kuna wanafunzi 11 waliopata ufaulu wa daraja la kwanza wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la pili 14 na ufaulu wa daraja la tatu wanafunzi 6. Amesema shule ya Floriani ina wanafunzi 8 waliopata daraja la kwanza, na wanafunzi 53 wamepata ufaulu wa daraja la pili, wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la tatu 61 na ufaulu wa daraja la nne ni wanafunzi 4 na wanafunzi 3 wamepata daraja sifuri.
Picha za matukio mbalimbali wakati wa ukaguzi wa ziara ya Afsa elimu
Ndugu Sijaona amesema ukiangalia uwiano huo wa ufaulu kuna ongezeko la ufaulu wa wanafunzi wa daraja la kwanza, la pili na la tatu ambao ni wengi kuliko waliopata daraja la nne na daraja sifuri. Ndugu Sijaona amesema shule ya Floriani ni shule inayochukua michepuo ya sayansi michepuo ya CBG na CBA. Ndugu Sijaona amesema Florian nayo bado inaendelea kusogea juu kwa ufaulu wa kitaaluma tofauti na wakati shule inaanzishwa, uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ulikuwa unasumbua maendeleo ya kitaaluma ya shule hiyo. Amesema kulikuwa na uhaba wa walimu wanaofundisha somo la kemia, tangu walimu wapelekwe shuleni, ufaulu umezidi kuimarika.
Picha za matukio wakati wa ziara ya afisa elimu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa