Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg. Charles.F.Kabeho alitembelea miradi saba ya maendeleo siku ya alhamisi. Baadhi ya miradi imewekwa jiwe la msingi, kufunguliwa , kutembelewa na kuzinduliwa.Miradi hiyo kwa ujumla imegharimu serikali takriban Tsh. 1,692,288,316.00.
Ndg. Charles alizindua shamba la vitungu lenye ukubwa wa ekari22, mradi huo ulizinduliwa na unatarajia kutoa mavuno yake Sep/10 hadi 15. Mradi huo umegharimu kiasi cha Tsh.233,620,000.00. katika uzinduzi huo Ndg. Charles alimpongeza mmiliki wa shamba hilo kwa kujenga mradi mzuri.
Ndg. Charles alifungua nyumba ya kuishi walimu katika sekondari ya Baray, mradi ulipata Tsh. 141, 000, 000.00 kutoka serikali kuu na Kutoka kwa Wananchi Tsh. 1,800,000.0.Hivyo kugharimu jumla ya 142,800,000.00. Pia alifungua ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Huduma ambapo serikali kuu ilitoa Tsh. 3,000,000,00 Halmashauri Tsh. 4,454, 000.00 Wananchi walitoa 48,940,000.00 na wahisani Tsh7,918,000.00. Hivyo kugharimu jumla Tsh.64, 312,000.00
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa aliweka jiwe la msingi katika kituo cha Kambi ya simba ambacho kilifanyiwa ukarabati ya majengo matatu na ujenzi wa majengo mapya kumi na tatu ambayo yamegharimu kiasi cha Tsh.651,000,000.00.Serikali kuu ilitoa kiasi cha Tsh.500,000,000 na Halmashauri ilitoa Tsh.89, 000,000 na Wananchi Tsh. 62,000,000.00 Pia jiwe la msingi limewekwa kwenye kiwanda cha kusindika mahindi ambacho kimepata Tsh. 42,560,000 kutoka serikali kuu na Halmashauri imetoa Tsh. 102,718,216.00 na kufanya jumla ya fedha zilizotolewa kwa mradi huo kuwa Tsh.145,278,216.00, Ndg. Charles Kabeho aliweka jiwe la msingi katika barabara ya NBC –Kudu yenye umbali wa km 0.6 katika mradi huo serikali kuu ilitoa 316,000,000.00
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa alitembelea mradi wa maji shule ya Ganako ambao Halmashauri ilitoa Tsh. 5000,000, Wananchi walitoa T.sh 5000,000 na Wahisani walitoa Tsh 139,278,100 hivyo kufanya jumla ya gharama kuwa 139,278,100. Mradi unaweza kutunza lita 10000 kwa saa na mradi unafanya kazi vizuri.
Ndg. Charles alitoa ujumbe wa mwenge uliosisitiza, wananchi katika sekta ya elimu kuendelea kutekeleza majukumu yao ya msingi kwa watoto wao. Serikali imeondoa michango na ada kwa shule za msingi na sekondari mpaka kidato cha nne. Wazazi wanapaswa kuwapa wanafunzi, sare za shule, madaftari, kalamu viatu na kuwapatia chakula wanapokuwa shuleni. Ndg. Kabeho amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya ukimwi, imeendelea kusisitiza watu kujua afya zao. Mpango wa sasa ni kuomba wanaume kujitokeza kupima na kupata ushauri nasaha, wanaume wamekuwa wagumu mno kujitokeza kupima.
Ndg. Kabeho amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya rushwa, rushwa ni adui wa haki ni vizuri kutoa taarifa kwa vyombo husika au kutumia namba 113 ambayo ni bure kwa mitandao yote. Ndg. Kabeho amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya malaria serikali inatoa vyandarua kwa kinamama wajawazito. Nivyema kujua matumizi sahihi ya vyandarua hivi. Ndg kabeho amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, ni vizuri wananchi wakaacha matumizi mabaya ya dawa za kulevya kwa sababu yanaongeza vitendo vya uhalifu na kurudisha maendeleo nyuma.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa