Mwenge wa uhuru umemaliza mbio zake katika mkoa wa Arusha na kukabidhiwa mkoa wa Manyara. Kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha mhe. Iddi Kimanta amesema mwenge wa uhuru umetembelea; umeweka jiwe la msingi, kufungua na kuzindua miradi 57 yenye thamani ya shilingi billion mia tano sabini na nane milioni mitatu na sitini na laki tisa na arobaini na tano elfu na senti hamsini.
Miradi kumi na nne kati ya kumi na tano imewekewa jiwe la msingi,miradi minne imefunguliwa na miradi kumi na mbili imezinduliwa. Mhe. Kimanta amesema miradi ishirini na sita itembelewa na kukaguliwa ili kuona maendeleo yake. Miradi iliyotembelewa ilikuwa ni ya sekta ya maji, afya, ujenzi wa barabara, elimu, utawala, kilimo, uvuvi na uhifadhi wa mazingira. Miradi miwili kati ya Hamsini na saba ilibainika kuwa na kasoro, mmoja ulikuwa ni wa kuwekewa jiwe la msingi na mwingine ulikuwa wa kutembelewa na kukaguliwa, yote ikiwa ni miradi ya maji.
Mhe. Kimanta amesema kiongozi wa mbio za mwenge ametoa maelekezo kwa miradi hiyo na Mhe. Kimanta amesema mkoa umeshaanza kuyafanyia kazi maelekezo ya kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa. Amesema baada ya wiki mbili maelekezo yatakuwa yamefanyiwa kazi na taarifa hiyo kupewa mkimbiza mwenge. Mhe. Kimanta amesema miradi iliyowekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za mwenge itafuatiliwa ili ikamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyolingana na thamani ya fedha. Mhe Kimanta amesema miradi iliyozinduliwa na kufunguliwa kwa matumizi mkoa utahakikisha miradi hiyo itatumika malengo yaliyokusudiwa inatunza na kuenziwa kwa tija kwa miaka mingi ijayo.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Kimanta amesema mwenge wa uhuru umeeendelea kusisitiza mapambano dhidi ya rushwa. Mwenge wa uhuru umeendelea kugusia juu ya athari za ugonjwa wa ukimwi, viongozi wa mbio za mwenge wamewaomba wananchi kuepuka tabia hatarishi kama ngono zembe ambazo zinaongeza maambukizi mapya ya ukimwi. Katika mikesha ya mbio za Mwenge wa uhuru, huduma za afya pamoja na ushauri nasaha zilikuwa zinatolewa. Mbio za mwenge wa uhuru umetoa elimu juu ya madawa ya athari ya dawa za kulevya, kupima vimelea vya malaria uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza huduma ya lishe.
Jumla ya unit za damu zilizochangiwa ni 134 walijitokeza kupima ukimwi 2323 wanaume 1570 wanawake753 waliokutwa na maambukizi ni 23 sawa 0.99%. walijitokeza kupima malaria ni watu 802 na wanaume 521 wanawake 281 waliokutwa na malaria ni watu 2. Mhe.Kimanta amewapongeza wakimbiza mbio za mwenge kitaifa wakiongozwa na Ndugu Mzee Mkongea Alli kwa kazi nzuri katika mbio za mwenge Arusha amesema wamekuwa wawazi na wakweli.
Kiongozi wa mbio za mwenge Ndugu Mzee Mkongea Alli ameshukuru uongozi wa mkoa wa Arusha kwa ushirikiano mkubwa. Lakini ameshukuru wananchi kwa muitikio walitoa kwenye mbio za mwenge mkoani Arusha. Ndugu Mkongea amesema ameona mambo mengi mazuri, wameona miundo mbinu ya madarasa, afya, na maji. lakini katika kipengele cha asilimia kumi ya kutoa mikopo kwa wananchi kimeendana na matakwa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa