Na Tegemeo Kastus
Haiwezekani kuendesha Halmashauri bila kukusanya mapato, Mamlaka ya mji mdogo lazima ifahamu inadhamana ya kukusanya mapato. Mambo yote yaliyopitishwa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo yanategemea mapato ya ndani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh, Abbas Kayanda katika kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha. Amesema lazima Mamlaka ya mji mdogo ikusanye mapato ili iweze kujiendesha vizuri na kufikia malengo waliojiwekea kwenye bajeti, kufanya hivyo kunasaidia mamlaka hiyo kuweza kujiendesha. Swala la kukusanya mapato si la madiwani wala watendaji pekeyao linapaswa kufanya kwa umoja. Amesema miradi ya ujenzi wa kituo cha afya kitakacho gharimu million 400, ujenzi wa ukumbi na kuboreshwa uwanja wa michezo yanategemea na jinsi Halmashauri itakavyojitoa kukusanya mapato ya ndani.
Matukio tofauti wakati wa kikao cha baraza la madiwani
Mh. Kayanda amegusia swala la ukusanyaji wa kodi ya majengo ambalo limerudishwa Halmashauri, amesema utekelezwaji wa swala hilo sasa utaanza kwa kuandaa mpango taarifa za majengo kwa kukusanya taarifa za majengo yote yaliyo katika Halmashauri ya Karatu. Zoezi la ukusanyaji wa kodi hiyo ya majengo linatarajiwa kuanza kufanyika mwezi wa nne. Amesema kumekuwa na kususua kwa watu kulipa kodi ya majengo, kodi hiyo inakusanywa na Halmashauri kwa niaba ya serikali kuu. Ametoa wito kwa watendaji kuelimisha wananchi ili waone umuhimu wa kulipia kodi ya majengo. Ameongeza kusema maendeleo ya nchi yeyote yanategemeana na uwezo wa nchi katika kukusanya kodi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. John Lucian amesema katika bajeti ya mwaka huu kituo cha afya kilichotengewa million 400 kitajengwa katika kata ya Buger. Amesema wamekubaliana kujenga machinjio ya ng’ombe Karatu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa machinjio ya kuku Karatu miradi ambayo ikikamilika itasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri.
Mh. Lucian amesema kitaaluma kwa mwaka ujao wa fedha wamelenga kununua mashine za kurudufisha makaratasi “Photocopy Machine” ikiwa ni pamoja na kufanyia ukarabati magari ili kuwezesha maafisa elimu kufanya ufuatiliaji wa maaendeleo ya kitaaluma kwa karibu. Amesema katika bajeti ijayo ya mwaka wa fedha wanafunzi kumi bora wa sekondari na wanafunzi kumi bora wa shule za msingi watatambuliwa na baraza la madiwani.
Mh. Lucian amesema kila afisa elimu amepewa kata yake ya kuilea kitaaluma ili kuongeza kiwango cha ufaulu. Lengo ni kupata mahusiano ya karibu kati walimu na watendaji wa wilayani katika kubaini na kutatua changamoto zinazodidimiza ubora wa elimu.
Madiwani wakiwa katika kikao cha baraza la bajeti
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa