Na Tegemeo Kastus
Fedha zinazotolewa na Halmashauri kwa ajili ya miradi ya maendeleo, Madiwani wa maeneo husika wapewe taarifa kwenye kata zao. Ukiwapa taarifa madiwani kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo kwenye kata zao inakuwa ni rahisi kuzifuatilia na kuzisimamia kwa karibu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. John Lucian wakati akifunga kikao cha kawaida cha baraza la madiwani. kilicholenga kufanya mapitio ya bajeti ya mwaka elfu mbili kumi na tisa na elfu mbili na shirini kwa kipindi cha miezi sita iliyopita. Amesema fedha asilimia arobaini kwa ajili ya maendeleo ya miradi ziende haraka kwenye maeneo husika. Amesema serikali imetoa fedha kiasi cha billion moja kwa ajili ya ujenzi wa majengo manne ya hospitali ya wilaya ameomba kuwe na kamati yenye uwazi katika usimamizi wa majengo. Amesema atateuwa madiwani wanne ambao kila diwani atasimamia ujenzi wa jengo lake. Amesema kuna fedha kiasi cha million mia na hamsini za ukarabati wa zahanati tatu lazima usimamizi wa hali ya juu ufanyike kuanzia kwa diwani wa eneo husika na viongozi wa chini.
Watendaji wakiwa katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani.
Mh. Lucian akizungumzia kuhusu mikopo inayotolewa na Halmashauri amesema ni vyema vikundi vikafanyiwa uchunguzi. Amesema kujiridhisha kunasaidia fedha kutopotea kwenye vikundi, amesema ikiwezekana fedha zitumike kununa vifaa vya uzalishaji badala ya kuwapa wanakikundi fedha hiyo itasaidia kupunguza matumizi mabaya ya fedha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Waziri Mourice akizungumza katika baraza hilo amesema vikundi hupewa fedha na Halmashauri ikiwa ni pamoja na muda wa miezi miwili kama kipindi cha matazamio kabla ya kuanza kurejesha mikopo. Amesema vikundi vya kinamama vinaongoza kwa kurejesha mikopo isiyo na riba kwa wakati kulinganisha na vikundi vya vijana.
Ndg.Waziri Mourice amesema vikundi vya vijana vinachangamoto ya kugawanyika pindi wanapopokea fedha. Hiyo husababisha vikundi kupitia wakati mgumu kuzirejesha fedha hizo. Amesema ni vyema sasa vikundi viwe vinaanza kutambuliwa kwenye ngazi ya kata husika.
Katika hatua nyingine Mh. Rehema amesema kuna umuhimu wa kuwashirikisha kwa karibu watendaji wa vijiji na watendaji wa kata katika kusaidia kusajili vikundi. amesema kama watendaji wa kata na vijiji wakihusishwa kwa karibu ni rahisi kufuatilia mikopo ya vikundi katika kata na vijiji vyao.
waheshimiwa Madiwani katika matukio tofauti wa kati wa baraza la Madiwani
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa