NA TEGEMEO KASTUS
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Mpya ya sekondari Eyasi na ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Domel.
Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa watendaji kuhakikisha ujenzi wa majengo unakamilika ndani ya muda uliowekwa na kuhakikisha ujenzi wa majengo unaendana na thamani ya fedha iliyotolewa. Shule mpya ya sekondari Eyasi ambayo ujenzi wa madarasa mawili unaendelea , ujenzi wake unafanyika kwa nguvu za wananchi na tayari Halmashauri imeshatoa kiasi cha million 10.
Mh. Abbas Kayanda (kulia) akiwa katika eneo linalojengwa madarasa shule ya sekondari Eyasi.
Katika shule ya sekondari Domel ambayo Madarasa na Bweni yanajengwa kwa fedha za serikali kupitia EP4R. Tayari uchimbaji wa msingi umefanyika na kusanyaji wa mawe umefanyika, Mh, Kayanda ameelekeza watendaji kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda wa siku tisini uliotolewa na serikali.
Mh. Abbas Kayanda akiwa katika jengo la choo linaloendelea kukarabatiwa katika mnada wa Qangnded.
Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa machinjio ya Mang’ola barazani inayoendelea kujengwa. Ujenzi wa machinjio hayo unatarajiwa kukamilishwa ndani ya muda wa siku saba. Mh. Kayanda ametembelea na kujionea ukarabati wa ujenzi katika choo cha Qangdend mnadani, maliwato ambayo awali yalikuwa yametelekezwa bila uangalizi wa viongozi wa kijiji. Maliwato hayo yanaendelea kufanyiwa ukarabati na tayari uongozi wa kijiji umeweka Mlinzi kusimamia usalama wa choo katika eneo hilo la mnadani.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa