Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu, ameambatana na watendaji wa Halmashauri kutembelea mradi wa soko unaojengwa. Maradi huo wa soko kwa sasa uko katika hatua ya uwezekaji wa paa.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Ndugu Waziri Mourice amesema lengo la kutembelea mradi huo ni kujionea ujenzi wa soko hilo. Ambalo amekuta mafundi wakiwa katika hatua za kuweka chuma juu upande wa kwanza wa soko na baada ya hapo wataendelea na upande wa pili wa soko. Ndugu Waziri amesema baada ya hapo wataezeka bati juu. Mkandarasi anafanya kazi kwa mda wa miezi mitatu kwa makubaliano ya kutengeneza nguzo na kuezeka bati. Amesema kwa mwaka wa fedha ujao wataendelea kwa hatua ya kutenga vizimba ndani ya soko. Lengo likiwa ni kuwawezesha wafanyabiashara waliopo nje ya soko kurudi ndani lakini pia kutengeneza vibanda vya chini. Vibanda ambavyo vikimalizika kutengenezwa vitapangishwa kwa wafanyabiashara na vitatozwa bei ya chini kati ya laki moja na laki moja na nusu.
Ndugu Waziri Mourice ametembelea eneo la jalala pia liliopo sokoni, amesema mazingira ya jalala si mazuri. Amesema uchafu ukiendekelea kubaki pale lilipo linaweza likaleta maradhi kwa wanachi. Amesema Halmashauri inafikiria kujenga jalala la kuweka uchafu nje ya pale lilipo kwa sasa. Kuondoa hali mbaya ya hewa iliopo katika eneo lile ili wananchi waendelee na biashara zao vizuri. Lakini pia kuondoa mbwa wa mtaani wanaozakaa katika jalala hilo la sokoni kujitafutia mabaki ya chakula.
Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Waziri Mourice pamoja na watendaji wakiwa eneo la ujenzi wa soko la Karatu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa