Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Abbas J. Kayanda tarehe 13/10/2021 alizindua mradi wa Maji, Maktaba, Madarasa na vyoo vya Wanafunzi shule ya Msingi Haydesh iliyofadhiliwa na shirika la World vision ,pia alishukuru kwa niaba ya Serekali kwa namna World vision wamekuwa wakifadhili miradi mingi ya maendeleo. Mkuu wa wilaya alielekeza fedha zote zitakazopatikana katika mradi huo wa maji zipelekwe Benki ili pindi matengenezo yanapohitajika iwe rahisi kufanyika na sio kusubiri mfadhili ,pia alielekeza Maktaba itumike vizuri ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya alipata nafasi ya kufanya mkutano wa hadhara Mang’ola Barazani lengo ni kusikiliza kero za wananchi . Wananchi walitoa kero mbalimbali za Maji, Umeme,na Upimaji wa Ardhi.
Kero ya Maji, Maji kutokufika Shule ya Sekondari Anagamazo, Kaimu Meneja wa RUWASA Ndg Ayoub Feswal alitoa ufafanuzi kuwa kwa kushirikiana na World Vision na Wakala wa maji Vijijini (RUWASA) kwa mipango waliojiwekea watahakikisha maji yanafika shuleni hapo.
Umeme, baadhi ya vijiji kutokufikiwa na umeme wa REA Mkuu wa wa Wilaya aliwaambia kwa sasa mkandarasi yupo maeneo mengine na kuwataka Wananchi wawe na subira watafikiwa na Umeme.
Upimaji wa ardhi, Mji wa Mang’ola unakuwa kwa kasi wananchi wanahitaji kupimiwa maeneo yao ili kuyapa thamani, Mkuu wa Wilaya aliwambia wananchi wataaalam wa aridhi walishafanya tathimini ya upimaji na kuwataka Wananchi kujitokeza kuchangia fedha kwenye Akaunti iliyofunguliwa ili wapimiwe kwa pamoja. Pia Mkuu wa Wilaya aliwaambia Wananchi Serikali imeleta fedha 1.6bil kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 58 vya madarasa kwa Shule za Sekondari.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa wananchi wa Karatu na kuahidi kusimamia matumizi ya fedha hizo kwenye ujenzi wa madarasa.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Abbas J. Kayanda akikakagua Mradi wa Maji katika Shule ya Msingi Haydesh
Mkuu wa Wilaya Mhe. Abbas J. Kayanda akikagua Mktaba ya kisasa Shule ya Msingi Hydesh
Mkuu wa Wilaya Mhe Abbas J. Kayanda akizindua madarasa Mawili ya Kisasa yaliyofadhiliwa na World
Vision
Mkuu wa Wilaya Mhe Abbas J Kayanda akizungumza nan a wananchi wa Mang’ola Barazani katika uwanja wa mikutano.
Mhe. Jacob P. Welwel Diwani Kata ya Mang’ola Barazani akifafanua jambo katika Mkutano wa mkuu wa Wilaya
Wananchi wa rika mbalimbali waliojitokeza katika mkutano wa Mkuu wa Wilaya
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa