Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Abbas J. Kayanda amefanya ziara ya kukagua miradi ya Afya na Elimu katika kata ya Rhotia katika ziara hiyo amekagua eneo la ujenzi wa Zahanati ya Rhotia kati lenye ukubwa wa ekari tatu, na kushauri Uongozi wa Kijiji kuzungumza na Mdau aliyewata eneo hilo Ndg.Safari Kwaaqw kuwapa upande unaopakana na barabara kwani si vizuri zahanati kukaa nyuma ya makazi ya watu.
Katika ziara hiyo alitembelea ujenzi wa Zahanati ya Kilima Moja iliyo jengwa kwa nguvu za Wananchi ambayo ipo hatua ya lenta, aliwapongeza Wananchi kwa kujitoa kwao. Katika ziara hiy alimuagiza Mganga Mkuu aingize zahanati hiyo kwenye mpango ili iombewe fedha za umaliziaji.
Pia katika ziara hiyo alikagua ujenzi wa Maabara ya Biologia shule ya Sekondari Kilimatembo ambao ulipata tsh 40mil kwa maksio mradi unaweza kukamilika kwa tsh 30mil fedha nyingine zitakazobaki zitumike kwenye maabara nyingine lengo la Serikali ni kukoa fedha. Mkuu wa Wilaya alionyesha kuridhishwa na hali ya ujenzi unaoendelea pia alishauri fedha hizo zitumike vizuri, maabara hiyo itakamilika tarehe 30/10/2021.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Abbas J. Kayanda katikati akiwa ameambatana na Mkuu wa Shule Hubert Mmbaga na Mtendaji wa Kata Sillo Dirangw wakielekea kukagua ujenzi wa Maabara.
Ndugu Manase Mushi akimwakilisha Mganga Mkuu Wilaya akifafanua jambo kwenya ziara ya Mkuu wa Wilaya.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa