Mkuu wa Wilaya Mhe: Abbas J. Kayanda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nagaibara
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe: Abbas J. Kayanda amefanya ziara kwenye Kijiji cha Ngaibara na Umbangw kata ya Kansay dhumuni ya ziara hiyo ilikuwa ni kupeana maelekezo kwenye Nyanja ya Elimu na Afya na kutatua Kero za Wananchi
Mkuu wa Wilaya alianza mkutano kwa kusikiliza kero za Wananchi, Kero kubwa hasa ilikuwa ni kero ya Maji, Umeme na Afya. Mtambo wa kusukuma maji unaoendeshwa kwa nguvu za umeme wa jua umepata hitilafu Mkuu wa Wilaya alielekeza mawasiliano yafanyike haraka fundi apatikane huduma ya maji iweze kurejea pia alishauri tatizo linapotokea taarifa zitolewe mapema ili ufumbuzi upatikane kwani wanaoteseka ni mama zetu wakiwa na mototo mgongoni kutembea umbali mrefu kufuata maji
Umeme, Mkuu wa wilaya aliwaambia wananchi makandarasi yupo maeneo mengine aliwahakikishia watafikiwa na huduma ya umeme na kipaumbele ni kwenye Taasisi za Umma na visima vya maji
Huduma ya Afya kutopatikana nyakati za usiku kutokana na Betri ya Sola kuharibika Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mganga wa kituo hicho Betri inunuliwe haraka huduma ya usiku irejee zahanati hiyo inahudumia asilimia 70 ya wakazi wa Ngaibara. Changamoto nyingine ni ukosefu wa vifaa vya Maabara Mkuu wa Wilaya ameelekeza vifaa vinavyohitajika viainishwe na vipatikane ndani ya mwezi huu. Pia ameshuri Wananchi wajitokeze kujiunga na bima ya Afya iliyoboreshwa. Vilele aliwahimiza Wananchi kujenga vyoo bora ili kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na kuwataka Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamia zoezi hilo dhumuni la Serikali ni kuhakikisha Wananchi wanakuwa na Afya bora.
Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya alitoa elimu juu ya Ugonjwa wa Uviko 19 na kuwasii Wananchi kujitokeza kuchanja kwani afya bora ni mtaji wa kila kitu.Mkuu wa Wilaya aliwaeleza Wananchi hao chanjo ni muhimu na salama ,chanjo hiyo ni kama chanjo nyingine haina madhara yoyote. Amewasii Wananchi kuchukua tahadhari na kupuuza upotoshaji uliopo kwenye mitandao ya kijamii.
Mkuu wa Wilaya alitembelea ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Umbangw ambayo yapo hatua ya umaliziaji na mengine hatua ya msingi, ameonyeshwa kuridhishwa na ujenzi unaondelea pia alishauri Karo la kuhifadhia maji lijengwe ili ujenzi uende kwa kasi.
Pia Mkuu wa Wilaya Alifanya ziara kwenye Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ambapo alikutana na wasimamizi wa mradi na Mafundi lengo likiwa ni kuharakisha ujenzi na kutoa maelekezo
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kansay Ndg. Nicola Matle akitoa elimu juu ya Umuhimu wa kupata chanjo ya Ugonjwa wa Uviko 19 kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya akiwa kwenye ziara ya kakakagua ujenzi wa Madarasa na ofisi Shule ya Msingi Umbangw pia alipata nafasi ya kuongea na Wazazi na kuhamasisha juu ya kupata chanjo ya Uviko 19.
Mkuu wa Wilaya Mhe Abbas J. Kayanda akikagua Mradi wa REA Kata ya Kansay ambao upo hatua ya usambazaji wa waya.
Mkuu wa Wilaya akielekeza jambo kwenye ujenzi wa Hospitali ya Wilaya alipokutana na baadhi ya wakuu wa Idara.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa