Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe Abbas J. Kayanda akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya , meneja wa maji wa KAVIWASU Stephen James Siay, Stanley Stephen meneja wa KARUWASA, Eng Mbaraka Kilangai Meneja wa RUWASA na Ndugu Simon Garaa Katibu mwenezi Wilaya na mjumbe wa Mkutano wa mkuu wa CCM Taifa ,alifanya ziara kwenye vyanzo vya maji vya Ngila na Bwawani lengo la ziara hiyo ni kuona hali ya uendeshaji na kuhakikisha wananchi wanapata maji.
Chanzo cha Ngila chenye visima Viwili, kimoja kikiwa na uwezo kuzalisha lita 35,000 kwa saa kingine , lita 10,000 kwa saa, chenye uwezo wa kuzalisha lita 10000 kwa saa kilipata hitilafu ya motor ambacho kinahudumia wakazi wa Kitongoji cha Tloma na NMC tayari motor nyingine ilishapatikana na mafundi wanaendelea na zoezi la kurudisha huduma ya maji.
Chanzo cha maji cha Bwawani, chenye visima viwili kila kimoja kina uwezo wa kuzalisha lita 35,000 kwa saa vinafanya kazi vizuri vinahudumia wakazi wa Karatu mjini na Gyekrum Arusha.
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ameelekeza operesheni maalum ifanyike ili kubaini watu waliojiunganishia huduma ya maji kiholela ili kuokoa upotevu wa maji. Vilel vile wamewasii Mamlaka za maji kuweka mazingira wezeshi ili wananchi waweze kujiunganishia maji, Mamlaka za maji zijitokeze kutafuta wateja wa huduma ya maji.
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ameshukuru kwa hatua za haraka zilizochukuliwa kuhakikisha huduma ya maji kwenye Vitongoji vya Tloma na NMC inarejea.
Mkuu wa Wilaya akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa maji wa KAVIWASU Stephen James Siay
Mkuu wa wilaya wa kwanza mbele akikagua chanzo cha maji cha bwawani
Meneja wa maji Karatu Mjini (KARUWASA) Stanley Stephen akionyesha jambo kwenye ziara ya mkuu wa Wilaya
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa