Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo aliwaongoza jana wananchi wa tarafa ya Endabash na watumishi wa Halmashauri kuchimba msingi wa majengo ya kituo cha afya tayari kwa kuanza ujenzi wa majengo mapya ya wodi ya watoto, wodi ya kinamama, wodi ya wanaume na jengo la upasuaji
Katika zoezi hilo aliungana na Mhe, Mbunge Willy Qambalo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Gerson Mnyenye, Katibu tawala wa Wilaya, Ndg Abbas Kayanda, Mkurugenzi Mtendaji,Ndg, Waziri .A. Mourice na Wakuu wa idara na vitengo kutoka Halmashauri ambao walishirikiana na wananchi waliojitokeza kuchimba msingi wa majengo hayo ya afya. Kituo hicho cha afya kimepewa million mia nne kutoka serikali kuu kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya zamani na ujenzi wa majengo mapya.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Mustafa Waziri amesema majengo mapya yanayotarajiwa kujengwa ni pamoja na Jengo la upasuaji (Theater), Nyumba moja ya mtumishi, Jengo la kufulia (Laundry) Maabara,Wodi ya watoto, na Tanuru la kuchomea taka. Majengo yatakayofanyiwa ukarabati ni wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, jengo la mama na mtoto (RCH) na ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje ( O P D) na kuweka mfumo wa maji.
Wananchi wamejitolea kubeba mchanga Lori arobaini na nane, mawe Lori mia arobaini na saba, kokoto Lori themanini na sita, na kuchimba msingi wa majengo hayo na serikali wametoa mafuta lita Elfu mbili na nyundo za kupasulia Mawe.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa