Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dadi H. Kolimba azungumza na baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kwenye Mkutano wa Kawaida uliofanyika tarehe 28/01/2022 kwenye ukumbi wa Halmashauri.
Mkuu wa wilaya amezungumzia mambo mbalimbali kuhusu mapato ya ndani,Afya, Elimu,miradi ya mendeleo na Wafanya biashara wadogo wadogo pia amewataka waheshimiwa madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano katika nyanja mabalimbali.
Mapato
Mkuu wa Wilaya amezungumzia uwepo wa mizani kwenye geti la kukusanyia ushuru wa zao la Vitunguu pia amesisitiza uboreshwaji wa kanzidata ya wafanyabiashara, ufuatiliaji wa leseni za biashara na matumizi ya EFD kwenye vituo vya Mafuta (petrol station). Aidha amesisitiza swala la ukusanyaji wa mapato ni muhimu sana ili Halmashauri iweze kutekeleza miradi ya maendeleo.
Miradi ya Maendeleo
Amesisitiza usimamizi wa karibu wa miradi ya maendeleo ili miradi iwe na viwango vinavyokubalika amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji kupanga Wahandisi vizuri wasimamie kila hatua ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.Amezitaka kamati za ujenzi kusimamia ipasavyo miradi ya ujenzi kupata bei halisi ya vifaa vya ujenzi.
Afya
Mkuu wa Wilaya alimuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha Dawa zinapatikana kwenye vituo vya Afya hii ni baada ya kupata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu ukosefu wa madawa.
Wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga)
Mkuu wa wilaya ameelekeza utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu kuwatengea wamachinga maeneo ya kufanyia biashara pia ameshauri kutenga fedha kwenye bajeti lengo ni kuhakikisha wanakuwa na maeneo mazuri ya kufanyia biashara
Elimu
Mkuu wa wilaya ameelekeza ufuatiliaji ufanyike katika zoezi la kuwaandikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza ili kuwabaini wale wote watakaoshindwa kuwaandikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza kwani miundombinu yote ipo tayari hakuna kisingizio.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa