Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Dadi H. Kolimba Amemshukuru Rais samia Suluhu Hassan Kwa Kuendelea kuboresha Huduma ya Elimu katika Wilaya ya Karatu na Taifa kwa Ujumla.
Mhe Kolimba Ametoa Shukrani hizo Leo March 18 2024 Katika Hafla fupi ya Utoaji Motisha kwa Waalimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mitihani ya Taifa 2023 wilayani Karatu.
"Niendelee Kutumia nafasi hii Kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kuendelea kuboresha Huduma ya Elimu katika wilaya yetu, tumeona ameendelea kujenga Shule Mpya na Kuboresha Majengo ya zamani Katika shule zetu za Msingi na Sekondari Tunamshukuru sana". Amesema Mhe Dadi.
Amewataka waalimu Wa shule zote za Sekondari na Msingi Kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kusimamia miradi hiyo na kuhakikisha wanazalisha Matokeo mazuri kwa wanafunzi katika shile zote.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Ndg. Juma Hokororo Ametumiq Hafla hiyo kuwahasa wazazi kuwa Mstari wa mbele kuwaunga mkono waalimu na serikali kwa ujumla Katika malezi bora ya watoto.
Amewahasa kushiriki katika shughuli muhimu zitakapo hitajika shuleni Kama vile kuchangia Michango ya Chakula Kushiriki katika vikao tajika shuleni ili kushirikiana pamoja Kufikia Katika malezi na Makuzi bora ya wanafunzi jambo litakalo changia Kuongezeka kwa Ufaulu wa Wanafunzi.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na Maji Ambae pia ni Diwani wa Kata ya Mhe. Ametoa Wito kwa Waalimu, Wazazi na Jamii kwa Ujumka Kusimamia Watoto/ Wanafunzi katika Janga la utandawazi ambalo ni sababu kubwa inayoweza kusababisha matokeo Mabaya kwa Wanafunzi na shule kwa Ujumla.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa