Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Abbas J. Kayanda jana tarehe 28/09/2021 amefanya ziara ya kukagua miradi ya Afya na Elimu katika kata ya Karatu mjini na Endabash,katika ziara hiyo amekagua Ujenzi wa Hospital ya Wilaya na kutoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtaka Afisa Manunuzi Wilaya kuhakikisha vifaa vyote vinanunuliwa kwa wakati na kufika eneo husika ili kuongeza kasi ya ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ameridhishwa na ujenzi wa Chumba cha Maabara ya Kemia Shule ya Sekondari Quaru katika ziara hiyo amekagua madarasa mawili na Ofisi ambayo yapo hatua ya upauaji na kuwataka waanze kufanya makisio ya fundi na pindi fedha itakapoletwa Tsh 25mil wahakikishe wanaisimamia vizuri.
Mkuu wa Shule Daniel A. Panga akitoa maelezo ya miradi ya Ujenzi kwa Mkuu wa Wilaya.
Gykrum Lambo Sekondari amekagua ujenzi wa choo ambacho kipo hatua ya lenta kinachojengwa kwa utaratibu wa kutumia ‘force Account,kwa lengo la kuokoa fedha za Serikali, kamati ya ujenzi imemuhakikishia ujenzi utamalizika ndani ya siku kumi na tano.
Mkuu wa Wilaya Mhe Abbas J. Kayanda akikagua ujenzi wa shimo la choo G/Lambo Sekondari
Gykrum Arusha Sekondari amekagua ujenzi wa choo matundu 12 ambao upo hatua ya lenta na kumtaka fundi kurekebisha kasoro zilizoonekana ujenzi utakamilika ifikapo tarehe 20/10/2021.
Ujenzi wa chumba cha madarasa mawili na ofisi Shule ya Msingi Gykrum Arusha ambao upo hatua ya jamvi ameridhishwa na ujenzi huo pia ameelekeza umwagiliwe maji ya kutosha ili uimarike vizuri.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa