Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi imetembelea mradi wa soko kuu la mjini Karatu, mradi ambao umefika katika hatua za upauzi. Sambamba na ukaguzi huo kamati hiyo imetoa muda kwa Halmashauri kukamilisha ujenzi kwa wakati ili kupunguza adha wanazopata wafanyabishara wa soko hilo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayaya Karatu ndugu Lucian Akonay amesema kuna taarifa kwamba soko hilo limetelekezwa na aliyepewa mkataba ndugu Anatory Construction amepewa mkataba wa kujenga soko kuu la mjini. Mkandarasi amekuwa na tabia ya kuondoka nje ya mradi mara kwa mara na kasi ya kupauwa soko hilo ni ndogo jambo linalokwamisha Wafanyabiashara ambao wanakaa sehemu ambayo si salama kufanya shughuli zao za biashara na kuna taarifa kwamba aliyepewa kazi ya kupaua soko hilo ameshindwa kutokana na ukadiriaji wa chini wa kazi. Ndugu Lucian amesema lazima tufanye maamuzi kwa maslahi ya wananchi ili mradi huo ukamilike kwa wakati.
Awali mkurugenzi mtendaji ndugu Waziri Morice amesema Anatory construction ilipewa tenda ya uzabuni wa vifaa katika soko hilo napia wamepewa tenda ya upauzi wa soko. Shughuli za ujenzi wa soko kuu mjini Karatu unatumia force accounts, amesema tenda ya upauzi inayohusisha Anatory constructions muda wake wa makubaliano umeisha tarehe 8/8/2019. Ndugu waziri amesema hata hivyo wakala huyo wa ujenzi alishaandikiwa barua ya onyo juu ya uwezekano wa kuvunjwa mkataba wake kutokana na kutokuwepo eneo la kazi bila taarifa ya mwajiri.
Picha ya juu ikionesha upauaji wa soko
Ndugu waziri amesema lazima ujenzi wa soko uendelee hata ikibidi kwa makubaliano na mafundi ili ujenzi uende kasi baada mkandarasi aliyepewa kazi ya upauzi Anatory constructions muda wake kufika kikomo kabla ya kufikia malengo ya mkataba. Ameongeza kusema anatambua wafanyabiashara waliokuwa wanafanya shughuli zao za biashara katika eneo hilo wanapata taabu sana hasa kipindi cha masika, malengo ni kukamilisha haraka kabla kipindi cha masika hakijawadia.
Injinia wa ujenzi wa Halmashauri ndugu Venance Malamla katika taarifa yake kwa kamati ya siasa amesema Mradi wa soko hilo ulitarajiwa kugharimu kiasi cha million 540 kwa makisio ya awali. Kutokana na mapungufu ya fedha mradi umegawanywa katika hatua mbili za ujenzi, hatua ya kwanza ilikuwa ujenzi wa nguzo na kupauwa jengo lote ambayo ingegharimu million 222. Hatua ya pili ni ujenzi wa sakafu, kujenga meza, kujenga ukuta wa nje kuweka miundo mbinu ya maji. Ujenzi wa soko ulianza mwezi wa tano mwaka 2018 na ulitarajia kukamilika mwezi wa sita 2019
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa