Na Tegemeo Kastus
Ufaulu wa shule za msingi mkoa wa Arusha unatakiwa kuanzia alama zaidi ya tisini na kuendelea kwa mitihani ya kitaifa. Mkurugenzi na Afisa elimu Msingi mnapaswa kulisimamia, lakini wazazi msimamie na mhakikishe watoto wanamahudhurio mazuri. Walimu mjipange katika kufundisha ili tuongeze kiwango cha ufaulu ili tusogee kwenda mbele baaada ya kuwa wa nafasi ya pili kitaifa kwa ufaulu mzuri.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Iddi Kimanta katika uzinduzi wa madarasa nane yaliojengwa na wadau wa maendeleo wa world vision katika shule ya msingi Endabash na madarasa mawili katika shule shikizi ya Endabash Salmay ikiwa ni pamoja na kuweka madawati. Ujenzi huo umegharimu kiasi cha zaidi ya million 558 ukijumuisha ujenzi wa vyoo vya watoto wakiume na wakike: ujenzi wa jengo la utawala, jengo la maktaba, ujenzi wa jengo wa jiko la kisasa na ukarabati wa madarasa matatu na mwaka huu wanatarajia kujenga madarasa mawili katika shule shikizi ya Endabash Salmay
Mh. Iddi Kimanta (katikati) akikagua miundo mbinu ya maji katika shule ya msingi Endabash
Mh. Kimanta amewapongeza shirika la world vision, amesema kuwa na mdau wa maendeleo wa namna hii lazima wananchi wajue kwamba ni fursa ya maendeleo, amesema wananchi wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuwaunga mkono shirika la world vision kwa kuwezesha utoaji wa elimu bora. Amesema namna ya kuwaunga mkono kwa wazazi ni lazima watoe mahitaji ya muhimu kwa wanafunzi ili waweze kusoma kwa bidii. Mh. Kimanta amewapongeza pia shirika la world vision kwa kusadia kujenga shule ya shikizi ya Salmay, amesema shule hiyo shikizi ya Endabash Salmay itasaidia kuondoa msongamano wa wanafunzi katika kijiji cha Endabash.
Akitoa salamu Mkuu wa wilaya ya karatu Mh. Abbas Kayanda amesema shirika la world Vision limekuwa likisaidai katika miradi ya afya elimu na maji, amesema kwa mwaka huu wa fedha wametenga kiasi cha billion moja na million mianane kwa mradi wa maji Endesh na miradi mingine ya afya katika Tarafa ya Eyasi. Mh, Kayanda ameomba wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na shirika la world vision, amesema serikali ya wilaya ya Karatu itaendelea kuwapa ushirikiano na kuwaunga mkono katika kazi wanazoendelea kuzifanya.
Mh. Iddi Kimanta akikagua miundo mbinu ya madarasa iliyojengwa na shirika la world vison katika shule ya msingi Endabash.
Awali katika salamu kwa wananchi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu Ndg. Waziri Mourice amesema shirika la world vision limetuokoa, kazi waliyoifanya ilipaswa kufanywa na Halmashauri na ingechukua muda mrefu kukamilika. Ndg. Mourice amesema shule ya msingi Endabash sasa hawana kizingizio cha kutofanya vizuri, kutokana na uboreshwaji wa miundo mbinu uliofanywa na world vision.
Msimamizi wa miradi ya world vision Tarafa ya Endabash Ndg. Goodluck Nnko amesema katika utekelezaji wa miradi ulikabidhiwa andiko lake liliandikwa mwezi wa 10 mwaka 2019 na ulianza kufanya kazi mwezi wa 7 mwaka 2020. Amesema lengo la mradi lilikuwa kutoa mchango katika kuboresha na kuandaa mazingira rafiki kufundishia na kujifunzia. Amesema mradi ulijikita katika kuwezesha upatikanaji wa maji safi, navituo vya vitatu vya kunawia mikono.
Ndg. Nko amesema mradi ulijenga matundu ya vyoo 18 kununu mashine ya photocopy yenye uwezo wa kurudufisha na ku-print aina ya canon, meza na viti 13 na madawati 286. Amesema mradi uliendesha mafunzo kwa kamati ya shule na kuwajengea uwezo katika usimamizi wa elimu na ukusanyaji wa rasilimali. Ndg. Nnko Amesema mradi utajenga kisima cha maji katika shule shikizi ya Endabash Salamay na kuboresha chumba kimoja cha darasa na kukifanya maktaba kwa kuweka samani na vitabu.
Katika taarifa yake Mkuu wa shule ya Msingi Endabash Mwl. Fredrick Maphie amesema shirika la world vision limewapatia kiasi cha computer 25 za wanafunzi na moja ya mwalimu. Amesema mradi umeongeza ari ya walimu katika ufundishaji na wanafunzi wameweza kuongeza ari ya kupenda kusoma. Amesema wanafunzi wamefanya kwa mara ya kwanza mtihani wa nusu mhula uliochapwa.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa kuweka kibao cha uzinduzi shule ya msingi Endabash.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa