Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amefanya ziara wilayani Karatu. Katika ziara hiyo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika kituo cha ukaguzi wa utalii Bashay na amefungua kituo hicho cha utalii pamoja na kukabidhi gari kwa jeshi la polisi litakalotumika kuwaongoza watalii kutoka (airport) uwanja wa ndege na kwenda kwenye hifadhi za utalii.
Waziri Mkuu Mhe.Kasim Majaliwa amepongeza ubunifu wa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kujenga vituo hivyo vinne vya utalii. Amesema ujenzi wa vituo hivyo unatija kwa wizara ya maliasili na utalii. Amesema kituo hicho ni kizuri kina mambo mengi na faida nyingi sana. Mhe. Kassim Majaliwa amempongeza pia wakuu wa wilaya na watendaji kwa kazi nzuri, amesema swala la utalii limepewa kipaombele kikubwa sana. Waziri Mkuu amesema serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa maelekezo sahihi aliyoyachambua kwenye ilani ya chama cha mapinduzi ambacho kinataka serikali isimamie; ipange itekeleze, na ijiridhishe sekta ya utalii inaendelea nchini ili faida zipatikane.
Mhe. Majaliwa amesema kuna utalii wa aina mbili, wa sisi wenyewe watanzania kwenda maeneo ya vivutio na wageni kutoka nje kuja kuona vivutio. Nchi yetu imebahatika kuwa na vivutio vingi sana, amesema tunafukwe nyingi na nzuri za mito na maziwa na bahari. Maeneo tuliyonayo ya vivutio ya Ngorongoro, Manyara Serengeti na mbuga nyingine. Mhe Kassim Majaliwa amesema vivutio vyote, serikali imeamua kuviratibu vizuri ili utalii uweze kufanyika.
Mhe.Kasim Majaliwa amesema serikali imenunua ndege 8, sita zimeingia ndege ya saba inakuja mwezi wa 10 na ndege ya 8 inakuja mwezi wa kwanza mwakani. Amesema Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amenunua ndege nyingine 3, amesema ndege zilizopo chini zinaruka na kwenda kila mkoa na wananchi wanasafiri kwa kutumia ndege zao. Mhe. Kassim Majaliwa amesema sasa wameanza kuwaita watalii na kwenda kuwachukua kwa ndege. Amesema ndege zetu zimeanza safari za kwenda India, China, Zambia, Ethiopia, Zimbabwe na Afrika ya kusini, amesema malengo yetu ni kuwavuta watalii kuja Tanzania moja kwa moja. Amesema zamani watalii walikuwa wanadanganywa kuhusu vivutio vyetu.
Mhe. Kasim Majaliwa amesema watu wengi wanakuja hapa Karatu, Arusha lazima tutumie kituo hicho kuweka vivutio ambavyo watalii watapenda kuviona na kununua. Amesema eneo lilobaki kwenye kituo wananchi wapate fursa wakae na wafanye shughuli zao za kitalii. Waziri mkuu amemshukuru, Mzee Joseph na mama Joseph kwa kutoa eneo la kiwanja kwa ajili ya kituo cha utalii. Amewapongeza wadau wa utalii kwa ujenzi wa kituo hicho cha utalii, amesema wamefanya kazi nzuri sana. Amesema hao ndio wanatoa taarifa nzuri kwa Tanzania na kufanya wageni wapende kuja Tanzania. Waziri mkuu amesema TATO na mawakala wote wa utalii wamefanya kazi kubwa sana. Amesema TATO wameleta watalii kutoka nchini Izrael 1000 kwa mara moja na wote wamekuja Karatu. Kuna watalii kutoka China ambao tayari wameshafika 360, na wiki ijayo wanakuja watalii wengine tena kutoka china watu 300 na watalii kutoka chini Izrael wapatao 400.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akiliwasha gari la waongoza utalii ambalo amelikabidhi kwa jeshi la polisi.
Mhe. Waziri Mkuu amesema serikali mwaka huu imeanza kuondoa kodi kwa waddau wa watalii ili wapate faida na wazidi kuwekeza. Amesema kufanya hivyo itasaidia wananchi kunufaika na Halmashauri kunufaika na shughuli za utalii pia. Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kuzidi kuchangamkia fursa za utalii na kuzidi kuboresha miundo mbinu ya hotel na tuhakikishe usalama wa watalii wanapokuwa katika safari zao za utalii.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo katika taarifa yake kwa Waziri Mkuu amesema; watu TATO wamefadhili askari kwenda kusoma kozi maalum ya kujifunza lugha, ili waweze kuhudumia watalii kwenye kituo cha utalii. Amesema kuna kituo kimejengwa KATITI wilaya ya Arumeru ambacho Halmsahuri ya wilaya hiyo walitoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo na kimejengwa kwa 90% na watu wa TATO, kituo kingine kinajengwa wilaya Longido na Halmshauri ya wilaya hiyo imetoa kiwanja, kituo kingine kimejengwa Monduli, Halmashauri ya wilaya ya Monduli imetoa kiwanja katika eneo la Makuyuni. Mhe. Mrisho Gambo amesema awali kabla ya ujenzi wa vituo hivyo watalii walikuwa wanasimamishwa kwa ukaguzi zaidi mara 20, jambo ambalo lilileta malalamiko kwa watalli wengi.
Mhe. Mrisho Gambo amesema watu wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongo wamejitolea kutoa wafanyakazi wa kudumu watakao fanya usafi katika maliwato ya kituo cha utalii Karatu. Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro itaweka kituo cha kutoa taarifa za utalii na kutakuwa na mtaalam atakayejihusisha na kutoa taarifa za utalii za hifadhi zetu katika kituo cha ukaguzi wa utalii Karatu. Mhe. Gambo amesema kuna wadau wa utalii wamejitolea kusaidia huduma ya internet kwa vituo vyote 4 vya ukaguzi wa utalii jambo ambalo litarahisisha utendaji kazi wa vituo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa