Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Luteni Josephine Paul Mwambashi ametembelea mradi wa barabara ya NBC-KUDU. Katika mradi huo Luteni Mwambashi amehimiza watendaji wa barabara kuendelea kuitunza barabara na kuhakikisha hakuna uharibifu wa miundo mbinu unaojitokeza.
Mradi wa barabara ya NBC-KUDU unamanufaa ya makubwa hasa katika Kupunguza matengenezo ya mara kwa mara, lakini umesadia huduma mbalimbali za kijamii kufikiwa kwa urahisi, kuboresha mandhari ya mji, kwa kuinua uwekezaji wa Utalii na kuboresha afya za jamii kwa kuondoa vumbi na tope.
Mradi huu wa ujenzi wa mita 600 za barabara ya NBC – Kudu kwa kiwango cha Lami uligharimu Shilingi 316,527,330 ambazo zilitolewa na Serikali Kuu kupitia Mfuko wa Barabara (Roads Fund). Kazi zingine zilizofanyika katika Mradi huu ni ujenzi wa mita 400 kwa ajili ya kupitisha maji ya mvua na Makalvati mawili (2). Mradi huu ulizinduliwa na Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa tarehe 12/06/2019. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kuutunza mradi huu kwa kuutengea fedha za usafishaji wa mitaro na matengenezo madogo yanayohitajika kutokana na matumizi ya Mradi.
Matukio mabalimbali katika picha wakati mwenge ulipotembelea mradi wa barabara
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa