Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Luteni Josephine Paul Mwambashi ametembelea mradi wa maabara ya computa katika shule ya sekondari ya Dr. Wilbroad Slaa. Luteni Mwambashi ametoa rai kwa wanafunzi kutumia vizuri elimu ya computa wanayopata kwa matumizi sahihi badala ya kujihusisha matumizi mabaya.
Mradi wa maabara ya computa katika shule ya sekondari Dr. Wilbroad Slaa umesaidia kuwaongezea wanafunzi maarifa ya msingi ya kompyuta (Basic computer Knowledge). Nakuweza kusaidia ufundishaji wakati upungufu wa vitabu vya kiada na ziada kwa waalimu na wanafunzi kwa kuweza kutumia mfumo huru usiotegemea mtandao (Student Offline System Study - SOSS) unaowawezesha wanafunzi kujisomea na kupata nukuu za masomo.
Shule ya sekondari Dr. wilbroad Slaa mwaka huu 2021, imefanikiwa kusajili baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha pili watakaofanya mtihani wa Taifa somo la kompyuta. Uendelevu wa mradi huu wa TEHAMA katika Wilaya yetu ya Karatu ni kutekeleza kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 isemayo "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu, itumie kwa usahihi na uwajibikaji".
Shule ya sekondari Dr. Wilbroad Slaa ilifanikiwa kupokea vifaa mbalimbali ambavyo ni Kompyuta thelathini na nne, Projector moja, Router moja, Switch moja na Samani zenye thamani ya 21,660,000/= kutoka kwa wahisani wa Ubelgiji chini ya taasisi binafsi ya DORIZON DOENJA na kubadilisha chumba cha darasa kuwa maabara ya Kompyuta.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Dr. Wilbroad Slaa akimuonesha kiongozi wa mbio za mwenge ambaye hayupo pichani namna tehama inavyowarahisishia kupata nukuu mbalimbali za masomo
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa