Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Luteni Josephine Paul Mwambashi amezindua mradi wa madarasa matatu katika shule ya sekondari Florian. Katika uzinduzi huo Luteni Mwambashi amesema kukamilika kwa ujenzi wa madarsa hayo kumeondoa adhaa ya mbanano wa wanafunzi darasani. Luteni Mwambashi ametoa rai kwa watendaji kuhakikisha miundo mbinu hiyo inatunza na kudumu muda mrefu.
Kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kumepunguza msongamano wa wanafunzi madarasani ambapo kwa sasa wanakaa wanafunzi arobaini darasani. Pia ufundishaji na ujifunzaji umekuwa rahisi kwa kuwa mwalimu anaweza kumfikia kila mwanafunzi kwa urahisi.
Mbio za mwenge wa uhuru zimeziundua mradi wa ujenzi wa madarasa matatu kwa gharama ya shilingi milioni hamsini na tano mia moja hamsini na tisa elfu mia tatu sitini na tisa na senti sitini na nane (55,159,369.68/=) tu na kubakiwa na kiasi cha shilingi milioni nne laki nane arobaini elfu mia sita thelathini na senti thelathini na mbili (4,840,630.32) tu ambazo zilifanyiwa mabadiliko ya matumizi na kutumika kwenye ujenzi wa choo.
Mradi wa majengo ya vyumba vitatu vya madarasa katika matukio tofauti ya picha
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa