Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Luteni Josephine Paul Mwamabashi ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Ayalabe. Amehimiza mkandarasi kuzingatia muda wa utekelezaji wa mradi wa maji kwa sababu maji ni hitaji la msingi la watu.
Mradi wa Ayalabe ukikamilika utazalishaji maji lita 744,000 kwa siku na kunufaisha wakazi wapatao 9,920 wa Kata ya Ganako.Ujenzi wa mradi huu mpaka kukamilika utagharimu jumla ya shilling za Kitanzania 599,131,583.00, mpaka sasa jumla ya shilingi za Kitanzania 268,354,267.00 zimeshapokelewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha kutoka Serikali Kuu, ambapo jumla ya Shilingi za Kitanzania 116,866,698.42 zimekwisha tumika na kupelekea mradi kufikia asilimia 40 ya utekelezaji.
Kazi ya usafishaji wa visima viwili na kupima wingi wa maji imekamilika kwa asilimia 100 na Ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 225,000 limekamilika kwa asilimia 100. Sambamba na ujenzi wa tenki (Sump tank) lenye ujazo wa lita 50,000 limekamilika kwa asilimia 100, Ujenzi wa “Pampu House” mbili mbili umekamilika kwa asilimia 95. Mradi umeshakamilisha mchakato manunuzi ya pampu tatu za kusukuma maji.
Matukio katika picha wakati kiongozi wa mbio za Mwenge alipotembelea mradi wa maji Ayalabe
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa