Jiwe la msingi katika jengo la Maabara katika kituo cha afya Endabash limewekwa na mbio za mwenge wa uhuru. Kiongozi wa mbio za mwenge Luteni, Josephine Paul Mwambashi amesema gaharama zilizotumika zinaendana na thamani ya jengo. Kiasi cha fedha kilichobakia kwenye bajeti ya ujenzi wa jengo hilo kiendelee kutumika mpaka ujenzi utakapoishia.
Ujenzi huo wa jengo la maabara unatarajia kuhudumia watu elfu sabini na mbili na mia mbili na sitini na nane kwa kupata huduma nzuri za vipimo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwaondolea usumbufu wa kusafiri umbali mrefu hadi mjini Karatu kutafuta vipimo. Pia kukamilika kwa mradi huo kutasaidia uongozi wa Kituo kuweza kutunza na kuhifadhi vifaa na vitendanishi vitakavyokuwa vinatumika kwa ajili ya kuendesha kitengo hiki cha maabara.
Hadi sasa ujenzi wa jengo la Maabara umefikia hatua ya umaliziaji. Kati ya Tshs. 41,540,000/= zilizotolewa na kupokelewa kutoka Serikali Kuu, hadi sasa zimetumika jumla ya Tsh 28,701,997.50 ambapo Tsh 22,222,997.50 zimetumika kununua vifaa vya ujenzi, na Tsh 6,479,000.00 ni gharama za ufundi. Fedha zilizobaki ni kiasi cha Tshs 12,838,002.50, ambapo Tsh 4,317,002.50 zitatumika kwa ajili ya kulipia vifaa vya ujenzi na Tsh 8,521,000 zitatumika kulipia mafundi na zuio la gharama za ufundi (retention fee) kwa hatua zilizokamilika.
Aidha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta alichangia kwa kutoa bati 65 na misumari kilo 20 zenye thamani ya Tsh 1,920,000 Vile vile wananchi walichangia nguvu kazi zenye thamani ya Tsh. 5,100,000 ikiwa ni kuchimba msingi, kubeba mchanga, kokoto,moram na mawe.
Halimashauri ya wilaya ya Karatu imesaidia katika kutoa wataalam kwa ajili ya usimamizi wa mradi huo ikiwemo kuwawezesha posho zao. Kutumia magari yake kwenye huduma mbalimbali kama kusafirisha wataalamu wake kwenda kwenye mradi ambayo ilihitaji mafuta.
Jengo la maabara katika kituo cha afya Endabashi lilowekewa jiwe la msingi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa