Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Luteni Josephine Paul Mwamabashi ameweka jiwe la msingi katika mradi wa soko kuu la Karatu. Luteni Mwambashi ameelekeza watendaji wa serikali kufanya mikutano na wananchi kuwaeleza hatua zilizofikiwa na mradi na mipango ya ukamilishaji wa ujenzi wa soko hilo.
kukamilika kwa mradi huu wa soko kutawawezesha Wakulima, Wafugaji na Wavuvi wa Karatu kupata sehemu ya kupeleka mazao yao kuuza kutokana na changamoto ya kutokuwa na soko la kuuzia mazao ambayo imekuwa ikiwakabili Wakulima, Wafugaji na wavuvi katika Wilaya ya Karatu ambayo asilimia 85 ya wakazi wake kujishughulisha na Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Soko hili litaongeza mnyoyoro wa thamani ya mazao kwa upande wa masoko. Mazao Makuu yanayotarajiwa kupelekwa sokoni ambapo kuna vizimba 2020 na vibanda 27 ni pamoja na Mahindi, Maharage, vitunguu, pia kuna mazao ya mifugo kama vile nyama, mayai na samaki. Pia wateja wanao nunua mazao mbalimbali watakuwa na sehemu moja ya uhakika ya kupata mahitaji yao kwa wakati mmoja. Soko hili vile vile ni chanzo cha mapato ya ndani ya Halmashauri kupitia kodi ya pango la vizimba na vibanda.
Ujenzi ulianza mwezi Aprili 2018, hadi sasa mradi huu umegharimu jumla ya Tsh 580,447,399.00 kwa mchanganuo ufuatao; Malipo ya mafundi ni Tsh 85,606,070.00 , Ununuzi wa vifaa vya ujenzi ni Tsh 485,883,329.00 na Mafuta ni Tsh 8,958,000.00
Mambo yaliyofanyika katika ujenzi wa soko hilo ni pamoja na ujenzi wa nguzo mlalo (beams) na nguzo wima (column); Upigaji wa makenchi yote na kupiga bati, Usukaji wa nondo kwenye nguzo mlalo (beams), nguzo wima (column) na slebu pamoja na umwagaji zege kwenye ghorofa,
Ujenzi wa mfereji wa kukusanya maji ya mvua, Jumla ya vizimba 202 vimejengwa, vimemiminwa zege la slebu, kuwekewa milango, kupigwa ripu na kupakwa rangi jumla ya maduka 27 yamejengwa na kupigwa ripu, Usukaji wa mfumo wa umeme kwa soko zima unaendelea bado kufunga mita ya umeme. Aidha kwa sasa kazi ya kuziba eneo la juu la soko kwa kutumia bati zinazoruhusu mwanga imekamilika.
matukio katika picha wakat kiongozi wa mbio za mwenge alipotembelea na kuweka jiwe la msingi mradi wa soko kuu karatu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa