Afisa elimu sekondari amefanya ziara jana katika shule ya sekondari Baray na Shule ya sekondari Qang’dend. Katika ziara yake alipata wasaha wa kuwaasa wanafunzi na kuzungumza na walimu lakini pia kuainisha mikakati yake ya kuinua kiwango cha taaluma.
Bi. Maina amesema tunahitaji matokeo makubwa wekeni mikakati kuondoa division zero, na F kwenye masomo. Tutekeleze majukumu yetu vizuri na tuwapende hawa watoto, amesema kupitia mikakati yetu tuliojiwekea tuinue kiwamgo cha ufaulu. Amehimiza walimu kujaza fomu za opras, amesema kila mfanyakazi atapanda daraja kutokana na matokeo ya utendaji kazi. Walimu tunahitaji kufundisha vizuri na ili tupate matokeo tunahitaji msukumo kutoka ndani.
Tuna mikakati ishirini na tano tuliojiwekea kuinua kiwango cha ufaulu lakini walimu mnambinu zenu pia za kufundisha zitumieni. Jitoeni kufundisha vizuri, matokeo ya form four na form two hayaridhishi. Bi, Maina amesema atafanya ziara za kushitukiza mara kwa mara ili kuona kama mikakati yake inatekelezwa vizuri. Amechukua changamoto mbalimbali zilizoelezwa na walimu na ameahidi kuzifanyia kazi.
Bi, Dorothea Singano Afisa Elimu Msingi aliyeambatana na Afisa Elimu Sekondari amehimiza walimu kufundisha kwa kiingereza ili wanafunzi waweze kujibu vizuri mitihani yao. Amesema mwalimu lazima uwe na haiba nzuri, kwa sababu wanafunzi wanaiga vitu kutoka kwa walimu wao. Amesema lazima mwalimu uvae vizuri mavazi ya kiofisi, mwalimu ni mzazi na mwalimu ni mlezi ni vyema tuwalee watoto vizuri. Walimu tuna wajibu wa kuwasadia wanafunzi kutimiza malengo yao, na tunapaswa tuwaongoze na kuwashauri wanafunzi vizuri.
Bi Dorothea amewaomba walimu kuondoa migogoro kazini, na kuwe na utaratibu mzuri wa kushauriana kuhusu kazi. Lazima kuwe na lugha nzuri za mawasiliano kati ya mkuu wa shule na walimu lakini pia walimu na mkuu wao wa shule. Walimu tusaidiane kutatua migogoro yetu wenyewe ili isiende mbali, lazima tufanye kazi kwa umoja. Lazima tufundishe kwa ufanisi na ufanisi wetu utaonekana kwenye ufaulu wa wanafunzi.
Bi Dorothea ameonya vitendo vya walimu kujihusisha na mapenzi na wanafunzi. Amesema mwalimu ni chachu ya mwanafunzi kupenda somo, tunawajibu wa kuwashauri wanafunzi. Tuwajenge wanafunzi ili watimize malengo yao na malengo yao yatatimia pindi watakapofanya vizuri kwenye mitihani yao.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa