Maadhimisho ya siku ya wanawake yamefanyika leo wilayani Karatu, kwa Maandamano ya amani ya wakinamama kutoka Halmashauri kwenda Uwanja wa mazingira bora. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo.
Maadhimisho hayo yameenda sambasamba na kujifunza mambo ya ukatili wa kijinsia; kujifunza ulinzi na usalama wa mtoto, Mada za ujasiriamali na mikopo, na Mada juu ya manufaa ya mfuko wa hifadhi ya jamii. Mhe Theresia Mahongo alipata wasaha wa kutembelea mabanda ya kinamama na kuhamasisha kinamama kuleta shughuli zao katika maonesho yao ili ziweze kuonekana na kujitangaza kwa umma.
Mhe. Theresia Mahongo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuwa wanawake kutumikia nyanja mbalimbali. Ushiriki wa shughuli za uchumi kwa mwanamke bado ni mdogo kutokana na mtaji mdogo na pia mila na desturi kandamizi. Kauli mbiu ya mwaka huu ya sherehe za wanawake ni, “badili fikra, kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu” Mhe. Theresia amesema kauli mbiu inalenga kuhamasisha jamii kwamba mwanamke ni muhimili wa maendeleo ya familia jamii na taifa kwa ujumla.
Mhe. Theresia amesema kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri imetoa kiasi cha Tsh. Million 423. Fedha hizo ni kwa mikopo ya wanawake na vijana amesema hicho ni kiasi kikubwa sana cha fedha. Mhe, Theresia amesema mikopo hiyo haina riba tofauti na taasisi nyingine za kifedha. Ameomba wale wanaopewa mikopo kurejesha kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika na mikopo hiyo. Amehimiza wanawake kuwa na bajeti katika matumizi yao ya kifedha ili wasitumie mitaji waliokopeshwa.
Mhe. Theresia amezionya taasisi za mikopo zinazochukua fanicha za ndani hasa wakati wanawake wanaposhindwa kurejesha mikopo. Amehimiza Taasisi hizo kuzingatia makubaliano, ni wajibu wa taasisi za mikopo kutoa red light. Tusiwafanye wakinamama wawe maskini kwa kuchukua vifaa vyao vya uzalishaji. Amehimiza taasisi za kifedha zinazotoa mikopo kupunguza riba, amesema wekeni riba nafuu ili muweze kufikia wanawake wengi.
Mhe. Theresia amewaelekeza dawati la kijinsia kushirikiana na ustawi wa jamii ili kupunguza matatizo yanayojitokeza kwenye familia. Amesema serikali inapinga shughuli za ukeketaji wa wanawake, amesema vitendo hivyo vina madhara makubwa kwa mwanamke. Wanawake tunapaswa kukataa unyanyasaji wa kijinsia na kukataa ukeketaji.
Mhe. Theresia amesema tunatakiwa kujisema wanawake wenyewe, kwa sababu hakuna ngariba mwanaume. Kuna dhambi tunazifanya tutakuja kuulizwa siku ya mwisho, amewaomba wanawake wa Karatu kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia. Wanawake tuwatunze watoto wetu wa kike ili wasiingie katika vishawishi. Mhe Theresia amewashukuru walimu kwa sababu walimu wanasaidia wazazi kwenye malezi. Tukipewa taarifa na walimu tusirudishe matusi, tushirikiane kulea watoto. Hii itasaidia hata mimba za watoto kupungua. Tuwafichue watu wanaotuharibia watoto wetu. Mwaka jana kulikuwa na wanafunzi 45 wa shule za sekondari na watoto wa 5 wa shule za msingi waliopata mimba.
Wakinamama wakiwa wamebeba bango lenye kauli mbiu ya siku ya wanawake.
Wakinamama wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe mbele ya mgeni rasmi.
Wakina mama wakiwa wamebeba mabango mbalimbali mbele ya mgeni rasmi.
Wakinamama wakiwa wameshika bango lenye ujumbe mbele ya mgeni rasmi.
Kinamama wakionesha bango mbele ya mgeni rasmi.
Akinamama wakionesha shamrashamra katika uwanja wa mazingira bora
Mhe. Theresia Mahongo akikabidhi hundi ya fedha kwa wakinama, fedha ambazo zimetolewa mkopo kwa ajili ya Wanawake na Vijana kupitia Halmashauri ya wilaya ya karatu.
Kinamama wakishiriki katika maandamano ya amani kuadhimisha sikukuu yao.
Kinamama wakipita katika mitaa mbalimbali ya mji kwa maandamano ya amani kusherehekea siku ya kinamama.
Haya ni baadhi ya maeneo maandamano hayo ya wanawake yalipita katika kuadhimisha siku ya wanawake.
Kinamama katika ubora wao, kwenye maandamano ya amani ya siku ya mwanamke.
Wafanyakazi wa Halmashauri wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Wakinamama walioshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Wakinamama wajasiriamali waliojiunga katika vikundi mbalimbali wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Kinamama maaskari wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Kinamama Waalimu katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi.
Wageni waalikwa katika siku ya wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa