Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ally ametembelea mradi wa maji Ganako, kuona undelevu wake katika utoaji wa huduma ya maji. Mradi huu wa maji ulizinduliwa tarehe 07 Septemba 2017 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2017 Ndugu Amour Hamad Amour.
Ndugu Mkongea ameridhishwa na mradi wa maji wa Ganako, amesema baadhi ya miradi imekuwa haidumu. Ndugu Mkongea amemuelekeza Mkuu wa wilaya kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu watakaojihusisha na kuharibu vyanzo vya maji na miundo mbinu yake.
Ndugu Mzee Mkongea akimtwisha mama plastiki ya maji alipotembelea mradi huo Ganako.
Mradi huu wa maji una kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 10,000 kwa saa, matenki 2 ya Lita 10,000 kila moja, Vituo 13 vya kuchotea maji (DPs), kati ya hivyo, 12 vipo Shuleni kwenye maeneo ya kusomea, bweni la Wanafunzi, Jikoni, nyumba za Walimu na 1 chenye midomo 3 kipo nje ya Shule kwa ajili ya Wananchi.
Mradi huu uligharimu jumla ya Shilingi 139,278,100/=, ambazo Wananchi walichangia Shilingi 5,000,000/=,Halmashauri shilingi 5,000,000 na mdau wa Maendeleo wa Shule yetu FOCTZ (Focus on Tanzania Community) kupitia Ndugu Richard Herriman alichangia Shilingi 129,278,100/=.
Mradi wa maji unahudumia wanafunzi takribani 741, walimu 31 na wananchi takribani 234. Mradi umeendelea kusaidia wanafunzi na wananchi wa jirani kuwa na uhakika wa Maji shuleni kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kupatikana kwa maji shuleni kumesaidia wanafunzi na walimu kupata muda wa kutosha wa kujisomea na kujifunza. Mradi pia umewezesha shule kumwagilia bustani kwa ajili ya mbogamboga, hivyo kuimarisha afya za wanafunzi na kuiongezea shule mapato kupitia uuzaji wa mbogamboga hizo. Huduma ya maji kupatikana hapa shuleni kumesaidia Wanafunzi kupata muda wa kutosha kujifunza.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa