Mradi wa Upendo katika kijiji cha Basodawish umetembelewa na kiongozi wa mbio za mwenge Ndugu Mzee Mkongea Alli. Mbio za mwenge wa uhuru umetoa cheti cha shukrani kwa taasisi ya Food for his children ambayo inafadhili na kusimamia mradi huo.
Ndugu Mzee Mkongea amesema mradi huo wa mbuzi unatija sana, mbuzi wanaofungiwa na kutunza kwa kupewa chakula inasaidia kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji. Amesema mbuzi na ngombe wanaoranda randa mtaani au wakati wa kuchunga wanaweza kuingia kwenye shamba la mtu. Ndugu Mkongea amesema kwa mfumo huo wa kufuga unaepusha mifugo kupatwa na magonjwa kama mbungo. Ndugu Mkongea ametoa tuzo ya shukrani kwa meneja wa mradi huo.
Awali meneja wa mradi huo Bi, Honorina Honorati amesema mradi huo ni moja kati ya miradi kumi. Amesema mradi huo umewawezesha wafugaji kujenga nyumba pia kupitia vikundi vyao wameweza kusomesha watoto wao na kujikopesha wao wenyewe. Bi, honorina amesema wamelenga kupunguza umasikini kwa kaya kupitia mradi wa mbuzi wa maziwa, mradi unampango mkubwa kwa miaka mitano ijayo kwa kuanzisha shamba lao kuzalisha mbuzi wenyewe.
Bi honoria honorati akipokea cheti cha alichokabidhiwa na mkimbiza mwenge kitaifa Ndugu Mzee mkongea
Taasisi hiyo imejikita katika kusaidia wananchi, wanafanya ufugaji bora na kupata uhakika wa chakula, afya bora na kuboresha kipato cha familia.Kikundi kilianza na wanachama 15 mwaka 2009 na kusajiliwa rasmi 06/03/2019 kikiwa na wanachama 47 na kupata namba ya usajili CSO.KRT/1842. Kikundi kilianza na jumla ya mbuzi 18 (mbuzi jike 15, madume 3). Hadi sasa kikundi kina jumla ya wanachama hai 47(wanawake 33 na wanaume 14), kimezalisha jumla ya mbuzi 292 (wapo mbuzi 172 na mbuzi 120 waliuzwa).
Kikundi cha UPENDO kimepiga hatua na kuongeza shughuli zingine za ujasiriamali kwa lengo la kuongeza pato la familia, kuweka na kukopeshana ambapo kina hisa za Shilingi 6,800,000.00 kwa kipindi cha miezi sita na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa watatu (jike moja mwenye mimba, ndama mmoja na dume mmoja) wenye thamani ya Shilingi 2,500,000.00
Mradi wa mbuzi umewezesha kuwa na manufaa kadhaa, Afya za familia zimeboreka kwa kutumia maziwa. Kuuza maziwa na kujipatia fedha za kuendeleza familia. Kuuza mbuzi na kujipatia fedha. Kuongeza mazao mashambani kwa kutumia mbolea ya mbuzi. Kupata elimu ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa, kilimo bora, elimu ya afya, elimu ya ujasiriamali. Mradi umewawezesha wakinamama waweze kujitegemea na kupunguza utegemezi wanaume. Mradi umerejesha amani ndani ya familia.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa