Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali ametembelea mradi wa ofisi ya kijiji cha Huduma kuona uendelevu wa mradi uliozinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2018 Ndugu Charles Francis Kabeho.
Ndugu Mzee Mkongea amesema ofisi inahitaji kuwekwa kifuniko katika chemba ya kutoa maji, amehimiza pia ofisi kuwa na daftari la taarifa za mahudhurio. Ndugu Mkongea amesema ni vyema kuwepo na daftari maalumu la kuomba ruhusa kwa wafanyakazi, lakini amehimiza pia ofisi kuwa na mafaili ya kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za ofisi. Ndugu Mkongea ameridhishwa na uendelevu wa mradi amesema ofisi ina miundo mbinu mizuri. Viongozi wa mwenge walishiriki kupanda miti katika eneo la mbele ya ofisi.
Ndugu Mzee Mkongea Alli akipanda miti mbele ya ofisi ya kijiji cha Huduma.
Ujenzi wa ofisi hiyo ulianza mwezi Januari 2016 na kukamilika agosti 2019. Ujenzi wa ofisi hiyo umegharimu shilingi 64,312,000 ambazo mchango wa serikali kuu ni shilingi 3,000,000 na Halmashauri ya wilaya shilingi 4,454,00, wadau wa maendeleo shilingi 7,918,00 na wananchi kupitia kaya 306 walichangia shilingi 48,940,000. Ofisi inavyumba saba vya ofisi kwa ajili ya wataalamu mbalimbali wanaotoa huduma na ukumbi mmoja wa mikutano.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa