NA TEGEMEO KASTUS
Matarajio yetu baada ya kuziba pande za pembeni sehemu ya juu zenye uwazi soko la Karatu litaanza kutumika ili wafanyabiashara waanze kufanya biashara katika mazingira mazuri. kumaliza ujenzi wa soko ni kipaombele chetu cha kwanza ili jengo lianze kutumika kwa wananchi, ingawa tunajenga mradi huu kwa mapato yetu ya ndani kulingana na bajeti ilivyowekwa na Halmashauri kwenye mwaka wa fedha.
Hayo yamesemwa na Mh. John Lucian Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu katika siku ya pili ya kikao cha baraza la madiwani, amesema soko la Karatu ni soko la kisasa ambalo mpaka sasa limeshagharimu zaidi ya million 500. Amesema Halmasahuri imefanya mchujo wa watu wanaotakiwa kufanya biashara kwenye vibanda hivyo utafanyika ili kuondoa mazingira ya udalali wa mtu kuchukua kibanda na kukikodisha kwa fedha ya juu kwa mfanyabishara mdogo wa soko. Kuna taarifa za baadhi ya watu waliokuwa wanamiliki vibanda zaidi vitatu kuanza kubadilisha majina ili kutengeneza mwanya wa kupata mkataba katika soko hilo jipya na llinaloendelea kujengwa.
Mh.Lucian amesema Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Karatu atafanya kikao na viongozi wa soko hilo na baadae kufanya kikao na wafanyabiashara wa soko hilo ili kujenga uelewa wa pamoja. Ikiwa ni pamoja na kupata wafanyabiashara wenye uhitaji wa kupata vibanda badala ya kupata orodha ya wamiliki ambao wanawapangishia wafanyabiashara. Mh. Lucian amesema mikataba ya muda itasainiwa ili kuweza kufanya tathimini kila wakati ya ili kujua idadi ya wafanyabiashara wenye uhitaji wa vibanda katika eneo la soko la Karatu.
Muonekano wa ndani soko la kuu la Karatu kwenye vizimba
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa soko Ndg, Waziri Mourice Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu amesema fedha za kuanza ujenzi wa soko zilipatikana wakati Halmashauri ilipotenga fedha kiasi cha million 220 kwa ajili ya kununua mitambo ya ujenzi wa barabara. Fedha hizo zilibaki baada ya serikali kusitisha kununu mitambo ya ujenzi wa barabara na badala yake kuunda wakala wa barabara vijijjini (Tarura). Hivyo fedha hizo kutumika kuanza ujenzi wa soko kuu la Karatu ambalo limeendelea kujenga kwa makusanyo ya ndani.
Ndg. Mourice amesema kazi zinazofanyika sasa ni kuziba nafasi za juu na kuweka bati za mwanga na kuweka mfumo wa umeme. Amesema tayari vibanda vimepigwa ripu na kupakwa rangi ili kuboreshwa muonekano na kumuwezesha mfanyabiashara kufanya shughuli zake bila kadhia yoyote. Amesema kuna vibanda vya chini ambavyo tayari vimepauliwa na ukuta wa juu katika upande wa vibanda vya chini vimwekwa waya ili kuruhusu hewa kupita ndani ya soko. Amesema vibanda vya juu ndio bado havijapauliwa mpaka sasa, amesema vizimba vya chini vipo 202 na vyumba 37 kai hivyo vyumba vya juu 10 havijamalizwa kuezekwa. Amesema ujenzi wa soko ukimalizika wataruhusu kwanza wafanyabishara wa vizimba 202 vya chini kuanza kufanya biashara huku wakiendelea kumalizia sehemu ya ujenzi zilizobaki.
Ameongeza kusema kunauhitaji wa fedha ili kuweka mabati ya mwanga na gata ili wafanyabiashara waanze kulitumia soko la Karatu. Ndg. Mourice amesema mfanyabiashara atakayeingia mkataba wa vizimba atapaswa kulipa kulingana na mkataba alioweka kwenye vizimba. Amesema katikati ya mwezi wa tano shughuli za kufanya wearing kuweka meshi na bati ya mwanga itakuwa imekamilika na wafanyabiashara wataruhusiwa kuingia, Amesema lazima upembuzi yakinifu ufanyike ili makosa ya kuweka watu wasio na wafanyabiashara yasijitokeze. Amesema kwenye list ya majina kuna changamoto ambayo inahitaji utatuzi wa haraka kabla ufunguzi wa soko haujafanyika.
wakati huo huo Ndg. Mourice amepongeza Halmashauri ya Karatu kwa kupata hati safi, amesema hilo limewezekana kwa sababu watendaji walitimiza wajibu wao vizuri. Ameshukuru pia baraza la madiwani kwa kuendelea kusimamia wataalamu vizuri jambo lilosababisha kupatikana kwa hati safi. Taarifa iliyotolewa na mkaguzi mkuu wa serikali katika Halamashauri 123 zilizopata hati safi na Halmashauri ya wilaya ya Karatu ilikuwepo. Amesema Halmashauri zilizokusanywa mapato chini ya asilimia hamsini, Halmashauri ya Karatu haipo, amesema katika kutenga fedha asilimia kumi za mikopo kwa wakinamama, vijana na walemavu Halmashauri ya Karatu imefanya vizuri.
Soko la kisasa linalojengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Karatu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa