Na Tegemeo Kastus
Ujenzi wa vyumba vya madarasa unapaswa kukamilika ndani ya wakati uliowekwa na serikali ili kuwezesha madarasa hayo kuanza kutumika.
Mkuu wa wilaya ya karatu Mh. Abbas Kayanda amesema hayo wakati alipotembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Baray Khusumay na Dr. Wilbroad. Amesema ni lazima wakandarasi waongeze kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili vyumba hivyo vya madarasa vianze kutumika kama ilivyopangwa.
Katika hatua nyingine Mh. Abbas Kayanda ametembelea shule ya sekondari Qurus na ameridhishwa na ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa vilivyojengwa katika shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda (kushoto) akikagua ujenzi wa Madarasa katika sekondari ya Qurus
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa