Sumu kuvu ni aina ya kemikali sumu inayozalisha ukungu au fangasi. Sumu kuvu inatokea kwenye mazao ya nafaka; mahindi, maharage, kunde na mbegu za mafuta. Shirika la afya duniani (WHO)katika taarifa yake limesema sumu kuvu huharibu karibu asilimia 25 au zaidi ya chakula kinachozalishwa duniani
Kuvu ni jina la kisayansi (Fungi) ambacho ni kiumbe hai, ambacho si mmea wala mnyama. Uanishaji wa kisayansi unavipanga katika himaya ya pekee ndani ya Eukaryota. Ekukryota ni kundi kubwa la viumbe hai ambavyo havina selli zenye kiini cha seli na utando wa seli. Wanyama, mimea, fungi wote tunaoona wanahesabiwa humo hii ni kwa mujibu wa (wikipedia)
Kuvu (fungi) katika matunda yanayooza
Afisa Kilimo Bi, Twilumba Ngwale amesema nchini Tanzania ugonjwa huu ulikuja mwaka 2014 na kuibuka tena mwaka 2016 mkoani Dodoma. Anasema sumu haionekani kwa macho, wala haina harufu, haina rangi wala kionjo hivyo kuwa jambo gumu kujua kama ugonjwa umevamia nafaka. Ukungu unaotokana na sumu kuvu unaweza kuwa rangi ya kijani ya chungwa, kijivu njano au kutoa harufu ya uvundo.
Afisa kilimo Bi, Ngwale anasema mazao yaliyohifadhiwa kwenye ghala kama yataathirika kwa kuliwa na wadudu, Mazao yanauwezekano mkubwa wa kuathirika na sumu kuvu. Anasema sumu kuvu huathiri sana nafaka zilizoanza kuathiriwa na wadudu kwa sababu inakuwa rahisi zaidi kupenya kwenye nafaka. Bi, Ngwale anasema mazao ambayo hayajakauka vizuri ambayo bado yana unyevunyevu nayo yanakuwa katika athari kubwa ya kuathirika na sumu kuvu.
Bi. Ngwale anasema mahindi kama hayajavunwa shambani na wadudu wakabangua yanakuwa katika hatare kubwa ya kushambuliwa na sumu kuvu. Lakini pia kama mkulima atavuna mavuno ambayo hayajakauka vizuri shambani nayo yanakuwa katika hatare ya kuathririka na sumu kuvu. Bi Ngwale anasema watu wa (ITTA) the International Institute of Tropical Agriculture walichukua sample za udongo ili kufanya utafiti wilaya Karatu kuhusu sumu kuvu na majibu ya utafiti huo bado hayajaletwa. Anasema kwa sasa inashauriwa kutumia Alsafa ambayo ni dawa ya kibailojia inayotumika kudhibiti sumu kuvu kwenye mazao. Inatumika wakati Mahindi yanapoanza kuchanua mbelewele. Bi, Ngwale anasema karanga ni zao linaloathirirka sanaa kwa sababu ni rahisi sana kwa unyevu kuingia, amesema hali ni hivyohivyo kwenye nafaka kama mazao hayahifadhiwi sehemu nzuri ni rahisi kuathirika. Bi, Ngwale anasema ni vyema wakulima wakahifadhi nafaka kwenye ghala linaloruhusu mzunguko wa hewa.
Bi, Ngwale anasema sumu kuvu inaweza kusababisha mtu kupata saratani ya maini, kwa sababu kemikali hiyo inapingia mwilini inaathiri sana maini. Amesema kemikali za sumu kuvu zinasababisha pia upungufu wa kinga kwa mwanadamu. Bi, Ngwale anasema sumu kuvu huathiri figo za binadamu na kuzorotesha ukuaji wa viumbe, binadamu na mifugo. Mazao yakiathirika na sumu kuvu inaathiri biashara ya mazao na matokeo yake ni soko la mazao kufa .
Bi ,Ngwale anasema namna ya kuepuka madhara ya sumu kuvu lazima mkulima avune mazao yakiwa yamekomaa na kukauka vizuri. Mkulima anashauriwa kutenga Mahindi yaliyoathirika na fangasi kwennye mahindi ambayo hayajaathrirka na fangasi. Bi, Ngwale amesema Mkulima anashauriwa ahifadhi Mahindi Maeneo yasiyo na Unyevunyevu. Mkulima anashauriwa asianike mahindi kwenye udongo badala yake atumie turubai au kichanja kuanika mahindi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa