NA TEGEMEO KASTUS
Nawapongeza shule ya sekondari Ganako kwa matokeo mazuri ya kidato cha sita, matokeo mazuri waliyopata yajenge ari kwa shule nyingine kufanya vizuri. Kiwango cha ufaulu kilichofikiwa na walimu wa Ganako sekondari ni vyema Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Karatu ukawapa motisha walimu ili wapate nguvu ya kujituma zaidi katika kazi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu, Mh. Abbas Kayanda katika kikao kazi na walimu wakuu wa shule za msingi, sekondari na waratibu wa elimu wa kata. Amesema kupata daraja la kwanza na la pili sio jambo la mchezo, kuna shule ya sekondari ya Agamazo nayo wamefanya vizuri nawapongeza kwa matokeo mazuri. Amekumbushia maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Arusha kwa Afisa elimu juu ya ufaulu wa kuanzia 90% kwa shulle zote za msingi,
kuwekewa mkakati maalumu katika utekelezaji wake.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza na walimu wakuu na waratibu elimu kata.
Kuhusu mbinu za ufundishaji Mh. Kayanda amesema walimu wanapaswa kuwafundisha wanafunzi kwa kutumia mbinu shirikishi ili kuwajengea uwezo mzuri wa uelewa wa masomo wanafunzi. Amesema bado walimu wanapaswa kuongeza maarifa katika ufundishaji, ukienda shule ya msingi kuna wanafunzi hawana kkk tatu za kuhesabu kuandika na kusoma. Lakini kuna walimu wanatoa mazoezi kwa wanafunzi lakini hawasahihishi jambo linalowapa wakati mgumu wanafunzi kujua usahihi wa majibu waliyoandika. Amesema kuna tatizo la walimu kutojiandaa kabla ya kwenda kufundisha, mwalimu anapaswa kuwa na mpango kazi ambao ni lesson Plann. Amesema lazima walimu watengenezee mazingira ya kuvutia ili mwanafunzi apende kwenda shule na kuwepo shule kila wakati.
Matukio katika picha
Akizungumzia utoro Mh. Kayanda amesema kuna utoro wa mwalimu kutokuwepo eneo la kazi au anaweza kuwepo eneo la kazi lakini asifundishe. Walimu huwa wanasoma somo la haiba ili kusaidia kujenga maadili katika ufundishaji lakini kuna baadhi ya walimu hawana lugha nzuri, tabia nzuri na wanavaa mavazi ambayo hayaendani na maadili ya taaluma ya ualimu. Amesema hayo mambo hayamsaidii kumjenga mwanafunzi kitaaluma. Mwalimu ni mtu muhimu sana katika kwenye jamii.
Wallimu wakuu na waratibu elimu wakiwa katika kikao.
Mh. Kayanda ametoa rai kwa miradi inayotekelezwa kwenye shule, amesema walimu kuwa makini na kujiepusha na ubadhilifu kwa fedha za miradi zinazojenga miundo mbinu ya elimu ili ziendana na thamani ya fedha iliyotolewa. Amesema ni vyema kufuata nyaraka na BOQ za ujenzi kama ilivyoelekezwa na serikali. Ameongeza kusema kuna taasisi za serikali hazina bendera wala picha ya rais, ametoa muda mpaka mwezi wa 8/30/2021 kila taasisi kuwa na bendera na picha ya rais.
Kuhusu kufanya kazi kwa ushirikiano Mh. Kayanda amesema walimu wakuu wanapaswa kufanya kazi na walimu wengine kama timu badala ya kugawa watu katika utendaji wa kazi. Amesema kuna wakuu wa shule wamekuwa wanafanya kazi kwa ubaguzi jambo linalokwamisha utendaji wa kazi. Walimu wakuu tumegeuza taasisi hizi kama mali zetu binafsi. Amesema ushirikiano unajengwa kwa ushirikiano wa pamoja na walimu wengine wa chini yako. Waalimu wakuu hawapendi kuulizwa mapato na matumizi ya shule zao, walimu wakuu wanapaswa kusiliza hoja za mtu katika kujenga jamii yenye uwajibikaji.
Ameongeza kusema hakuna mwalimu amesomea ukuu wa shule, hivyo kusimamia watu ni kazi lazima wakuu wa shule muweze kuwa na vifua vya kuishi na walimu wasaidizi wenu. Amesema kuna shughuli ndogo ambazo mkuu wa shule anapaswa kuagiza mwalimu mwingine wa kawaida kwenda. Badala ya kung’ang’ana kila kitu uende mwalimu mkuu, tujenge tabia ya kuwaachia walimu wengine watekeleze majukumu . Amesema mwalimu msaidizi akifanya jambo zuri, mwalimu mkuu onesha appreciation.
Matukio katika picha
Akizungumzia kuhusu ufadhili wa Wei Bantwana Mh. Kayanda amesema utekelezaji wa ufundishaji wa somo la komputa kwa shule ambazo walimu walipewa mafunzo ya ufundishaji wa computa katika shule tisa ni shule sita zimefanikiwa kusajili wanafunzi kufanya mtihani wa kidato cha pili. Ameelekeza shule ambazo zina masomo ya komputa zihakikishe mwakani zinafanya usajili wa wanafunzi kidato cha pili. Dunia imebadilika na tuko kwenye ulimwengu wa sayansi na technolojia, amesema kuna komputa mpakato 120 nyingine zitatolewa na wafadhili aina ya apple kwa shule za sekondari.
Matukio katika picha
Amesema sambamba na hilo shule za sekondari kwa kushirikiana na wadau wa elimu Wei Bantwana watasaidia kuratibu mtihani wa ndani wa wilaya. Amesema kuna timu ya wataalamu ambayo itafanya mapitio ili kuja na njia za kufanya mtihani huo kwa ushindani, ametoa wito kwa walimu watakaoingia katika utungaji wa maswali kuwa na waaminifu ili kuepusha kuvujisha mitihani hiyo kwa wanafunzi.
Mh. Kayanda ametoa rai kwa walimu kuepuka mikopo hatarishi, amesema kama mwalimu unataka mkopo basi tukope kwa kiasi. Badala ya kujenga tabia ya kukopa kwenye taasisi za mtaani ambazo zinalazimisha mteja kuacha kadi ya bank. Jambo hilo ni hatare kwa usalama wa fedha za mteja, akizungumzia uhamisho Mh. Kayanda amesema kumekuwa na maombi ya kuhama kwa walimu wengi wanaoishi maeneo ya pembezoni kuja mjini. Ameomba walimu kukaa kwenye vituo vyao vya kazi ili muda wao wa kutoka ukifika waondoke. Mpango wa serikali ni kuboresha mazingira ya kazi kila sehemu.
Matukio tofauti wakati wa kikao
Akizungumzia majukumu ya waratibu wa elimu kata Mh. Kayanda amesema haridhishwi na utendaji wa waratibu elimu kata. Amesema utendaji wao wa kazi umeshindwa kumsaidia Afisa elimu katika shule wanazozisimamia. Amesema afisa elimu kata lazima awe mtatuzi na mfumbuzi wa changamoto zilizo katika kata na mambo ambayo yako nje ya uwezo wake basi anapaswa kufikisha kwa afisa elimu. Amesema lazima waratibu elimu wawe na mpango kazi wa kusimamia na kufuatilia taasisi za elimu zilizo katika eneo lake la kiutendaji
Mh. Kayanda amezungumzia muongozo wa serikali uliotolewa ili kukabiliana na Covid-19, ametoa rai kwa watendaji kufuata maelekezo ya serikali kikamilifu. Shule ziwe na ndoo za maji tiririka na vitakasa mikono ili wanafunzi waweze kunawa na kujikinga kwa kutumia vitakasa mikono.
Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Waziri Mourice akizungumza na wakuu wa shule na waratibu elimu kata.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Karatu amesema ni vyema watendaji wakafanya kazi kwa kufuata utaratibu. Amepongeza sekondari ya Ganako kwa kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita, tafsiri ya kufaulu kwa kiwango hicho ni kwamba wanafunzi walielewa badala kukariri na hiyo imechagizwa na usimamizi mzuri wa walimu.
Amesema walimu ni walezi na mwanafunzi katika ukuaji wake kwa sababu wanatumia muda mwingi wakiwa na mwalimu, hivyo jamii kubwa inalelewa na mwalimu, ameomba walimu kuendelea kuwalea wanafunzi vyemaa. Amesema tabia za jamii kwa kiasi kikubwa inajengwa kutokana na misingi ya bora na imara ya malezi ya walimu kwa wanafunzi wanapokuwa shuleni.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa