Kikao cha baraza la Mamlaka ya mji mdogo wa Karatu kilichokuwa kifanyike siku ya leo kimeahirishwa kwa muda usiojulikana. Kikao hicho kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti Ndugu Elisifa Boa kimevunjika baada ya wajumbe kutaka kulipwa malimbikizo fedha zao.
Kikao hicho ambacho kilipaswa kuanza kusikilizwa saa nne asubuhi, kilichelewa kuanza kwa mda uliopangwa. Baadae kuanza katika hali ya kuchelewa saa tano asubuhi, baada ya kufunguliwa na mwenyekiti wa Baraza la mamlaka ya mji mdogo ndugu Elisifa Boa. Mwenyekiti alianza na ajenda ya kwanza ya kufungua kikao ambayo ilifanyika kati ya ajenda nane za kikao hicho cha kawaida cha Baraza la mamlaka ya mji mdogo. Hali ilibadilika baada ya moja ya mjumbe kuomba kupata muafaka wa fedha wanazodai kwa muda wa miezi mitatu na vikao tisa vilivyofanyika.
Ndugu Joseph Lollo amesema kwa hali jinsi ilivyo wanaanza kukosa imani na Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo, amesema ni vyema kikao cha baraza la mamlaka ya mji mdogo kiahirishwe imefika wakati wa kupaza sauti. Baada ya hoja hizo Mwenyekiti aliwaomba wajumbe kupiga kura ili kuridhia hatua za kuahirisha kikao. Wajumbe wengi walipiga kura ya kuahirsha kikao, Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo ndugu Elisifa Boa alifunga kikao.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu ndugu Waziri Mourice amesema kweli amekutana na Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo, Makamu mwenyekiti na Afisa Mtendaji mamlaka ya mji mdogo. Amesema katika kikao chao kilichofanyika Ofisi ya mkurgenzi mtendaji kuanzia mda wa saa tatu na nusu mpaka saa nne wamejadili hali ya ukusanyaji wa mapato yaliyochini ya mamlaka ya mji mdogo.
Ndugu Waziri Mourice amesema kuna kiingilio cha uwanja wa mazingira bora ambayo mpaka sasa wana 37 % tuna mwezi mmoja tu tumalize mwaka hizi asilimia zilizobakia zinakusanywa kwa utaratibu gani ? ili kutimiza malengo ya bajeti. Amesema ushuru wa taka Mamlaka wa mji mdogo kupitia wenyeviti wa mtaa wanapaswa kushirikiana na Mtendaji wa mamlaka kukusanya fedha hizo. Amesema walipaswa kukusanya million mia moja ishirini na moja laki moja na sabini na sita. Amesema mpaka sasa wamekusanya million sitini na tisa sawa na 57% kuna 43 % zinapatikana wapi ??
Ndugu Waziri Mourice amesema kuna ushuru wa nyumba za kulala wageni wamekusanya 49 % ambao ni sawa na shilingi million 36 tuu. Ndugu Waziri amehoji 51% inapatikana wapi ?? Mkurugenzi mtendaji ndugu Waziri Mourice amesema ni lazima tufanye vikao vienye ufanisi, Wenyeviti wanapaswa kushirikiana na watendaji wa Mamlaka ya mji mdogo kukusanye fedha. Ndugu waziri amesema lazima tukubali kuwajibika kufanya kazi ili tulipwe, ndugu Waziri amesema yeye anasimamia utaratibu.
Ndugu Joseph Lollo akichangia katika kikao cha kawaida cha Mamlaka ya mji Mdogo Karatu
Wajumbe wakifuatilia hoja katika kikao cha Mamlaka ya mji Mdogo
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa