Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha ameendelea kupokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani. Ndugu Saanare amewaapisha wanachama hao wapya na kuwapa kadi za chama cha mapinduzi wanachama zaidi ya 200 .
Miongoni mwa watu waliopokewa wapo madiwani wawili wenyeveviti vijiji vya Endagem Endabash, Ngaibara na Laja. Lakini pia chama cha mapinduzi kimepokea na kuwapa kadi wajumbe wa vijiji na wanachama wengine wapya waliojiunga na chama. Ndugu Erasto Sanare Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha amesema amefarijika na mabadiliko wanayofanya watu wa Karatu.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Karatu Ndugu Lucian Akonay amesema zaidi ya miaka 25 Karatu imekuwa haina maendeleo. Maendeleo lazima yafuate muunganiko wa ngazi za uongozi; kuanzia Mwenyekiti wa mtaa, Diwani, Mbunge na Rais, diwani pekee yake hawezi kuleta maendeleo kwa wananchi. Amesema ukichanganya viongozi wa vyama tofauti katika ngazi hizo inaleta changamoto katika utendaji wa kazi.
Ndugu Lucian amesema katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji, ccm itafanya kampeni za kistarabu na kutoa elimu kwa wananchi. Amesema anataka viongozi watakao chaguliwa kutoa taarifa za mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu. Amesema sasa ccm itafikisha madiwani 14 kutoka madiwani 4 iliyokuwa nao kwenye uchaguzi mkuu.
Mhe.Joseph Martin aliyekuwa diwani wa Oldean amesema ameunga mkono juhudi za raisi,kutokana na kazi aliyoifanya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amesema mambo aliyoyafanya huwezi ukalinganisha na kipindi miaka kumi iliyopita. Amesema ukitaka kujenga uchumi lazima ujitoe sadaka kwa kuchagua kilicho sahihi kwa wakati huo, ili baadae umalizie kujenga kilichobakia. Amesema huwezi kumlinganisha Mlaji na Mzalishaji kama hujajenga miundo mbinu sahihi kama anayoifanya rais, ya kujenga standard Gauge, ujenzi wa barabara, Stigler George, kununua Ndege na kuimarisha viwanda. Wananchi sisi ni walaji na tunajihusisha na kilimo bidhaa zetu ili zifikie viwandani tunahitaji barabara nzuri reli viwanja vya ndege ili na Mlaji apate bidhaa za viwandani kama biskuti mikate kwa bei rahisi. Amesema baadae output ya viwanda kwa maana ya faida ndio inatumika kujenga miundo mbinu ya huduma za kijamii kama hospital na shule. Amesema uchumi wa Tanzania unaimarika vizuri na Mhe. Rais Magufuli anatumia vizuri rasilimali za nchi.
Mhe. John Pissa aliyekuwa diwani wa Kansay akikabidhi kadi yake ya chama kwa Mwenyekiti wa ccm mkoa Ndugu Sanare
Mhe. Josephat Martin aliyekuwa diwani wa Oldeani akieleza sababu za yeye kujiunga na ccm.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa