Na Tegemeo Kastus
Kikao kazi cha bonde la kati kimefanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri, kikao hicho kililenga kuwajengea uwezo watendaji wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama juu ya sheria za usimamizi wa maji. Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mheshimiwa Theresia Mahongo alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho.
Katika hotuba yake ya ufunguzi Mheshimiwa Theresia amesema maji ni muhimu katika maisha ya binadamu na ndio maana tunasema maji ni uhai, katika maisha yetu maji yakikosekana hayana mbadala. Maji hutumika katika matumizi ya manyumbani, na yanatumika katika matumizi ya viwanda. Mheshimiwa Theresia amesema bila maji hakuna samaki, mradi mkubwa wa Stigler George unategemea maji na ni mradi utakaokuwa na gharama nafuu, uchimbaji wa madini unategemea maji na hata shughuli za usafiri majini zina gharama nafuu.
Mheshimiwa Theresia amesema robo tatu ya mwili wa binadamu ni maji, amesema kiasi cha maji kilichopo chini ya ardhi kimepungua na hii imetokana na uharibifu wa mazingira, ongezeko la shughuli za mifugo ambao wanatumia maji, ongezeko la watu na kuchoma misitu. Mifugo imesababisha vyanzo vya maji kufukiwa kutokana na mmonyoko mkubwa wa udongo. Ongezeko la watu imekuwa changamoto katika matumizi ya maji kutosheleza mahitaji. Amewaomba watendaji kusimamia na kutunza vyanzo vya maji, amesema sisi tunatunza chanzo cha maji cha ngorongoro ambayo sisi ndio tunatumia.
Mheshimiwa Theresia amesema kukosekana kwa maji kwenye hifadhi ndio kunasababisha wanyama kutoka kwenye hifadhi na kuja kwenye makazi ya watu kutafuta maji. Amesema sera ya maji (2002) inataka usimamizi shirikishi kupitia jumuiya za watumia maji, ili kuepukana na migogoro ya maji. Amesema kuna kijiji kama Matala kuna visima 8 vya maji ambavyo havitoi maji amemuelekeza Injinia wa maji wa wilaya kushughulikia swala hilo. Tufanye kazi ya kuelimisha wananchi kuelewa sheria za usimamizi rasilimali maji na kuzuiya uchafuzi wa maji hasa ukizingatia nchi inaenda kwenye uchumi wa kati ikiwa ni pamoja na kuzuia uchimbaji wa visima usioratibiwa.
Mheshimiwa Theresia ameomba wizara maji kutenga fedha kwa ajili kumalizia kuweka mipaka ya kudumu kwenye vyanzo vya maji, zoezi hili lilianza (2016) lakini kutokana na matatizo ya kifedha lilishindwa kumalizika. Mheshimiwa Theresia Ameomba wizara pia kusakafia mifereji inayotiririsha maji mang’ola. Mifereji iliyosakafiwa haifiki hata km 10 amesema mang’ola kuna km 80.3 za mifereji ambazo hazijasakafiwa, amesema kama wilaya wako tayari kufanya budget reallocation. Amewaomba wakulima wa mang’ola kuanza kuweka fedha kwenye mfuko kwa ajili ya kusakafia mifereji hiyo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa