Maadhimisho ya siku ya wauguzi yaliyofanyika katika kituo cha afya Mbuga Nyekundu, yamefanyika kwa ufanisi mkubwa. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni wauguzi mbiu inayoongoza afya kwa wote.
Dkt. Mustafa Waziri amesema Karatu inawatumishi wa idara ya afya 356 kati ya 746 wanaohitajika kuna uhaba wa watumishi 390 wa idara ya afya. Amesema idara ya afya ina 52 % ya upungufu wa watumishi na ina 48% idadi ya watumishi walioajiriwa. Dkt Mustafa amesema kuna changamoto kubwa ya watumishi, lakini bado idara ya afya inaendelea kupambana kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt.Mustafa amesema amekuwa akitekeleza zoezi la kuhamisha watumishi ili kukidhi mahitaji ya huduma kwa wananchi, amesema kwa sasa kila kituo cha afya kina watumishi wasiopungua watatu.Dkt Mustafa, amesema anaendelea kulipa madai ya watumishi wa kada ya uguzi, amesema watalipwa kwa awamu na awamu hiki kiasi cha milioni 5 na laki 8 kinachodaiwa na wauguzi kitalipwa. Fedha hizo ni laki 1 na 20 elfu kama fedha za sare za kazi. Dkt. Mustafa amesema kwa watumishi wanaotaka kujiendeleza kimasomo kuna utaratibu mzuri wa kujiendeleza ili mradi mfanyakazi afuate utaratibu huo na yeye kama Mganga mkuu wa wilaya ataridhia. Amesema swala la motisha; kila kituo kipange motisha kwa watumishi wake, amesema asilimia 15 ya makusanyo yanayofanywa kwenye kituo ya fedha yanabaki kwenye kituo na hilo lipo kwenye miongozo. Lakini pia kwa watumishi wanaokaa mbali kama Matala watatumia gari la kituo cha afya Mbuga Nyekundu kuja mjini wanapokuja kuchukua mshahara. Amesema idara ya afya imewapa pikipiki watumishi wa Matala na Ginamilanda.
Dkt, Mustafa amesema bado wanaendelea kutatua changamoto za nyumba za makazi za watumishi wa afya. Amesema zahanati ya Endesh, kulikuwa na mtumishi alikuwa ameweka makazi ndani ya zahanati amesema mwezi huu ni wa mwisho kwa mtumshi huyo kuendelea kuishi pale.Diwani wa kata ya Baray kwa kushirikiana na Mganga mkuu wa wilaya wamemtafutia nyumba mtumishi huyo katika nyumba za makazi za wafanyakazi kwenye moja ya shule. makazi ya nyumba wamepewa pia watumishi wengine wawili waliopangiwa katika zahanati hiyo. Amesema idara ya afya iliweka bajeti ya million 10 ya kujenga nyumba kwa kushirikiana na wananchi, Dkt Mustafa ameshukuru mkuu wa wilaya kwa kuweka mkazo kwa fedha hizo kwenda katika zahanati hiyo. Idara ya afya imeendelea kuwapandisha vyeo na kuwabadilishia muundo wa utumishi wafanyakazi wake.amesema kuna watumishi takribani 53 wamebadilishiwa mshahara na watumishi 9 wamebadilishiwa muundo wa Utumishi.
Wafanyakazi wa Idara ya afya wakiwa na nyuso za furaha kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi kituo cha afya Mbuga Nyekundu.
wauguzi wa Afya wakiwa kwenye maandamano katika sherehe za siku ya wauguzi zilizofanyika Mbuga Nyekundu.
Matukio mbalimbali ya maandamano ya siku ya wauguzi yaliyofanyika kituo cha afya Mbuga Nyekundu.
Picha za matukio mbalimbali wakati wa maandamano ya wauguzi kituo cha afya Mbuga Nyekundu.
Picha za mabango tofauti katika maadhimisho ya siku ya wauguzi kituo cha afya Mbuga Nyekundu.
Picha ya bango ikionyesha kauli Mbiu ya siku ya wauguzi, iliyofanyika kituo cha afya Mbuga Nyekundu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa